Loading...

Hii hapa maana halisi ya 'Valentine Day' inayoadhimishwa Tarehe 14 February kila mwaka

Ilikuwa kipindi cha karne ya tatu dola ya kirumi ilikuwa chini ya mtawala Claudius II mtawala huyu aliamuru vijana wote wasioe bali waajiriwe katika jeshi la warumi, kwa yeye aliamini kuwa vijana ambao hawajaoa ni askari shupavu katika vita kwa kuwa hawatakuwa na majukumu ya kifamilia.

Lakini kipindi hicho miaka ya 270 Baada ya Kristo yaani (270 AD) alikuwepo Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki alijulikana kwa jina Padre, Valentine kasisi huyu hakuridhika na amri ya mfalme Claudius wa Pili ya kutokutaka vijana wasioe badala waajiriwe katika jeshi.

Hivyo Padre, Valentine kwa kutokuridhika kwake na amri ya mfalme akawa anawafungisha vijana ndoa kwa usiri mkubwa ili asijulikane na utawala, lengo lake ni kuwanusuru vijana dhidi ya ngono zembe nje ya ndoa kwani kwake yeye aliitafsiri kama dhambi kubwa mbele za Mungu.

Kadiri siku zilivyozidi kwenda huku Padre Valentine akiendelea kufungisha ndoa kwa siri, mtawala Claudius wa pili alibaini kuwa idadi ya vijana jeshini inapungua na baada ya utafiti aligundua kuwa vijana wengi walifungishwa ndoa kwa siri kisha kuanza kujikita katika kutunza familia zao na kutelekeza amri yake ya kuwa vijana wasioe bali wahudumie jeshi.

Baada ya kubaini mtawala huyo alitoa amri ya kukamatwa kwa Padre, Valentine kwa kukiuka amri ya mfalme, Padre Valentine alikamatwa na kufungwa Gerezani, akiwa gerezani alipata vijana wengi waliomtembelea pale gerezani wakitambua kazi aliyokuwa akifanya Padre, Valentine kuwanusuru vijana wasifanye Zinaa kwa kuwafungisha ndoa tena kwa siri kinyume na amri ya Mfalme.

Kabla ya kuhukumiwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa Padre, Valentine aliandika waraka kwa binti mmoja ambaye alikuwa anampenda sana kwa kusema From your Valentine yaani kutoka kwa Valentine, kuanzia hapo mpaka leo hilo neno likashamiri siyo tu kwa Wakristo tu bali kwa walimwengu wa imani, rangi na maeneo yote. Kwa tafsiri ya historia hii Padre, Valentine ni muasisi wa familia kwani alitamani kuona vijana wakiishi katika maisha ya familia badala ya kufanya zinaa.

Baada ya Historia hiyo fupi ya Siku ya Wapendanao sasa tujiulize maswali haya: Je, siku hizi yanachofanyika siku ya Valentine day yanaakisi maana halisi ya siku hiyo?

Siku hiyo iliasisiwa kwa heshima ya Padre, Valentine aliyetamani vijana wasifanye zinaa wakamchukiza Mungu, Je, hilo linazingatiwa? Kwa tafsiri kwamba siku hiyo kwa tafsiri ya siku hizi inaitwa siku ya Mapenzi?

Tumshukuru Mungu kwa Ajili ya Padre, Valentine ambaye pia baadaye kanisa lilimtangaza kuwa Mtakatifu. Zaidi tulifuate lile lililokuwa kusudi lake hasa kuishi maisha ya familia

Tunakutakia siku njema ya VALENTINE msomaji wetu!!!
Hii hapa maana halisi ya 'Valentine Day' inayoadhimishwa Tarehe 14 February kila mwaka Hii hapa maana halisi ya 'Valentine Day' inayoadhimishwa Tarehe 14 February kila mwaka Reviewed by Zero Degree on 2/14/2017 03:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.