Mfanyakazi wa wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi apandishwa kizimbani kwa tuhuma za Rushwa.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imempandisha katika kizimba cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kigogo mmoja kutoka wizara ya elimu ,sayansi, teknolojia na ufundi, Angelus Kapinga kutokana tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.
Katika shtaka ya kwanza kapinga anakabiliwa na shtaka la kuomba rushwa ya sh.milioni mbili kwa mmiliki na mkurugenzi wa shule za FK, Fares Mero huku katika shtaka lingine anakabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya sh.milioni moja kwa mmiliki huyo.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi mkuu Wilbard Mashauri,wakili kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Denis Lekayo alieleza kuwa katika kosa la kwanza mtuhumiwa huyo alilitenda februari 2, 2015 ambapo akiwa mwajiriwa katika wizara hiyo aliomba rushwa ya sh.milioni mbili kwa Mero ili amsaidie kuzifungua shule za FK zilizofungwa na wizara kutokana na kuendesha biashara hiyo kinyume na taratibu.
Alieleza katika shtaka la pili, ferbuari 2, 2015 mtuhumiwa akiwa eneo lisilojulika jijini Dar es Salaam alipokea rushwa ya sh.milioni moja kupitia M-pesa kwa akaunti namba 0754281880 kutoka kwa mero.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo hakimu Mashauri aliharisha kesi hiyo hadi machi 7 mwaka huu ambapo itakuja kwaajili ya mtuhumiwa kusomewa maelezo ya awali.
Februari 15 mwaka huu vigogo wanne wa wizara hiyo walipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa saba ya uhujumu uchumi ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya sh. Milioni 41.
Mfanyakazi wa wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi apandishwa kizimbani kwa tuhuma za Rushwa.
Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2017 02:15:00 PM
Rating: