Loading...

Mtuhumiwa wa mauaji ya kaka wa kiongozi wa korea kaskazini alilipwa dola 90

Siti Aisyah, mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya nduguye kim Jong un
Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.

Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.

Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa.

Maafisa wa polisi wa Malaysia wanasema wataanza kufagia uwanja huo wa ndege ambapo shambulio hilo lilifanyika siku 12 zilizopita ili kuchunguza sumu yoyote iliosalia.

Maafisa wa polisi wa Malaysia walivamia nyumba yake huko Kuala Lumpur mapema wiki hii ili kuchunguza mauaji hayo.

Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ,huku washukiwa wengine saba waisakwa na polisi ikiwemo raia wanne na Korea Kaskazini.

Source: BBC Swahili
Mtuhumiwa wa mauaji ya kaka wa kiongozi wa korea kaskazini alilipwa dola 90 Mtuhumiwa wa mauaji ya kaka wa kiongozi wa korea kaskazini alilipwa dola 90 Reviewed by Zero Degree on 2/25/2017 08:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.