Loading...

VIDEO: Samatta anavyoendelea kung'ara nchini Ubelgiji

MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta juzi usiku alirejea uwanjani na kuifungia KRC Genk bao moja kwenye ushindi wa bao 3-0 walioupata dhidi ya mahasimu, Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

Samatta aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza tangu aumie mgongo Februari 1, alifunga bao lake dakika ya 39 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo raia wa Hispania, Alejandro Melero. 

Pozuelo alimsetia Samatta bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Saint Truiden.

Mabao mengine ya Genk kwenye mchezo huo yalifungwa na Melero na Ruslan Malinovskiy.

Mchezo wa mwisho Samatta alicheza kwa dakika 23 tu baada ya kuumia walipocheza dhidi ya KV Oostende na kufungwa bao 1-0. Mchezo wa juzi ulikuwa wa 41 kwa Samatta tangu asajiliwe na timu hiyo.


VIDEO: Samatta anavyoendelea kung'ara nchini Ubelgiji VIDEO: Samatta anavyoendelea kung'ara nchini Ubelgiji Reviewed by Zero Degree on 2/12/2017 01:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.