Loading...

AUDIO: Kauli iliyotolewa na TFF baada ya TRA kuzifunga ofisi zao

Shirikisho la soka nchini TFF limekiri kudaiwa mamilioni ya shilingi ambayo yalitakiwa kulipwa kama kodi katika mamlaka ya mapato TRA ambayo March 15, 2017 ilizifunga ofisi za shirikisho hilo kwa shinikizo la kulipwa kwa fedha hizo.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema ni kweli deni hilo lipo na limesababishwa na shughuli mbali mbali za mchezo wa soka ambazo ziliwahi kufanyika hapa nchini miaka ya nyuma.

Alfred amesema mzigo mwingine wa deni ambao umeongezwa katika akaunti ya TFF umesababishwa na mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans kupitia mchezo wao wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe ambao ulichezwa mwaka 2016.

“TFF inadeni la muda mrefu, kwa hiyo inabidi tunakae na serikali kuona namna ya kuweza kulitatua kwa sababu hili deni linatokana na kodi iliyotokana na ujio wa timu ya taifa ya Brazil mwaka 2010 wakati huo uongozi wa sasa haukuwepo madarakani.”

“Kama mnakumbuka wakati ule serikali ilimleta kocha wa timu ya taifa kutoka nje, ikawa inamlipa mamilioni ya pesa lakini TFF ikijua kwamba anakatwa kodi hukohuko lakini haikuwa hivyo. Kodi nyingine ongezeko lake liliibuka mwaka jana kwenye mechi kati ya Yanga na TP Mazembe mchezo uliochezwa June 28 ambapo Yanga waliwaruhusu mashabiki kuingia uwanjani bure kwenye mechi hiyo.”

“Licha ya mashabiki kuingia uwanjani bure, lakini walipigiwa hesebu kulingana na idadi yao. Serikali haiitazami moja kwa moja klabu, badala yake inaibana TFF. Sisi tuliamua kubeba deni lile ambalo ni zaidi ya bilioni moja.”

“Tulijitahidi kulipa deni la kodi za Maximo hadi kufikia nusu hadi kufikia mwezi uliopita, lakini wamekuja tena bila kutupa notes wanataka tukubaliane kwamba tutakuwa tunalipa kiasi gani kila mwezi au kila wiki.”

“Kwa sasa TFF haina pesa kwa sababu inamajukumu mengi kama mnavyojua timu ya Serengiti ipo kambini kuna timu ya soka ya wanawake. Tunajitahidi kwa kiasi hicho kidogo kinachopatikana kukigawa sehemu mbalimbali na hadi sasa ofisi imeshafunguliwa.”




Source: ShaffihDauda
AUDIO: Kauli iliyotolewa na TFF baada ya TRA kuzifunga ofisi zao AUDIO: Kauli iliyotolewa na TFF baada ya TRA kuzifunga ofisi zao Reviewed by Zero Degree on 3/17/2017 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.