Loading...

Pogba kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Midlesbrough wikendi hii [Video]

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba hataweza kuchezea klabu hiyo mechi ya Ligi ya Premia Jumapili ugenini dhidi ya Middlesbrough.

Hii ni baada yake kupata jeraha kwenye misuli ya paja.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia kipindi cha pili cha mechi ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kati ya United na FC Rostov ya Urusi na ikamlazimu kuondoka uwanjani.

Nafasi yake ilijazwa na Marouane Fellaini.

Manchester United walishinda 1-0 kupitia bado la Juan Mata na wakasonga hati robofainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Rostov.

Pogba, 24, pia anatarajiwa kukosa pia mechi za timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Luxembourg na Uhispania baadaye mwezi huu.

Meneja wa United Jose Mourinho hakusema Pogba anatarajiwa kukaa nje muda gani.

Alipoulizwa iwapo huenda ikawa karibu wiki tatu, Mourinho alisema: "Kweli. Lakini sina uhakika, lakini kwa kweli hawezi kucheza dhidi ya Middlesbrough na hatachezea timu ya taifa."

Pogba ndiye mchezaji aliyenunuliwa ghali zaidi duniani na amefungia United mabao saba na kusaidia ufungaji wa mengine matano katika mechi 41 alizowachezea msimu huu.

Mholanzi Daley Blind pia alilazimika kuondoka uwanjani kutokana na kilichoonekana kuwa jeraha lililotokana na kugongwa.

Hata hivyo, hali yake kamili haijaelezwa.

Mata aipeleka United Robo Fainali ya Eropa Ligi


Manchester United wamesonga mbele na kuingia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kuifunga Rostov 1-0 katika mchezo wa raundi ya pili uliochezwa Old Trafford. United wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1.

Juan mata ndio alifunga bao hilo pekee katika mchezo ambao United walionekana kupata tabu kuvunja ngome ya Rostov. Manchester United wangeweza kusonga mbele hata kwa matokeo ya 0-0 kwa kuwa tayari walikuwa na goli la ugenini.

Wasiwasi kwa mashabiki wa Manchester United pengine ni kuumia kwa kiungo wao Paul Pogba ambaye hakumaliza mchezo, kutokana na kuumia msuli wa paja. Nafasi yake ilichukuliwa na Marouane Fellaini.

United walitawala mpira lakini hawakufanikiwa kupata chochote hadi katika dakika ya 70 ambapo Mata alifunga bao hilo la ushindi.

Katika mechi nyingine mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta aliisaidia timu yake kuingia robo fainali dhidi ya KAA Gent licha ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.


Pogba kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Midlesbrough wikendi hii [Video] Pogba kukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Midlesbrough wikendi hii [Video] Reviewed by Zero Degree on 3/17/2017 12:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.