Loading...

Baraza la Sanaa la Taifa [Basata] limeufungia wimbo wa Nay wa Mitego

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeufungia rasmi wimbo "Wapo" wa msanii Elibariki Emmanuel maarufu kama Nay wa Mitego.

Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Mngereza amesema hayo leo (jumatatu) na kueleza kuwa wimbo ulioimbwa na msanii huyo usitumike kwa namna yoyote ile kwa kuwa umevunja sheria ya Sanaa.

Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Mngereza
"Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L)cha sheria ya Basata namba 23 ya mwaka 1984,baraza limepewa jukumu la kusimamia kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali zisizo salama, "alisema Mngereza.

Aidha Baraza limewaonya wale wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi.
Baraza la Sanaa la Taifa [Basata] limeufungia wimbo wa Nay wa Mitego Baraza la Sanaa la Taifa [Basata] limeufungia wimbo wa Nay wa Mitego Reviewed by Zero Degree on 3/27/2017 01:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.