Loading...

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye 'kukamatwa' kwa tuhuma za rushwa

Waendesha mashtaka wamesema wataomba idhini ya kumkamata aliyekuwa rais wa taifa hilo Park Geun-hye, kwa mchango wake katika kashfa ya ulaji rushwa nchini humo.

Alipoteza kinga ya rais dhidi ya kufunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng'oa madarakani.
Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa.

Bi Park amekanusha madai hayo.

Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.

Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".

Wanasema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa.

Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.

Park aling'olewa vipi madarakani?

Bi Park aliondolewa madarakani kutokana na uhusiano wake wa karibu na Bi Choi.

Bi Choi (kati) anatuhumiwa kujihusisha katika ulaji rushwa
Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia jamii ambazo alikuwa anazisimamia.

Kaimu mkuu wa kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung, Lee Jae-yong, alikamatwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Bi Park, 65, anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika hili, na kwamba alimruhusu Bi Choi uhuru wa kiwango kisichokubalika wa kufikia nyaraka rasmi za serikali.
Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye 'kukamatwa' kwa tuhuma za rushwa Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye 'kukamatwa' kwa tuhuma za rushwa Reviewed by Zero Degree on 3/27/2017 01:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.