Mahakama ya juu nchini Korea kusini yamwondoa madarakani Rais Park Geun-hye
- Wabunge Korea kusini wapiga kura kumuondoa Rais Madarakani.
- Rais wa Korea Kusini, Park Geun Hye agoma kuitikia wito wa mahakama.
Mahakama hiyo ya kikatiba imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuharibu demokrasia.
Park ambaye ndio mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo alihusishwa na kashfa ya kujipatia fedha kwa njia za ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini humo na rafikiye mkubwa Choi Soon-Sil.
Bi Park huenda akakabiliwa na mashataka ya uhalifu.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yalio na wapinzani wa rais huyo.
Lakini wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili.
Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60.
Rais huyo sasa amepokonywa uwezo wa kutoshtakiwa na sasa anaweza kusimamishwa kizimbani na kufunguliwa mashtaka.

Wapinzani wa Park Geun Hye walisherehekea uamuzi huo katika barabra za mji wa Seoul |
Bi Choi wakati huohuo ameshtakiwa kwa kuchukua hongo kwa madai ya kuyashinikiza makampuni makubwa kumpa pesa huku akiahidi kwamba kampuni hizo zitapendelewa na serikali.
Bi Park ameshtumiwa kwa kushirikiana na Choi.
Jopo la majaji wanane katika mahakama ya kikatiba liliangazia mashtaka yanayomkabili bi Park na kuamua kwamba kulikuwa na sababu mwafaka za kumwachisha kazi.
Wafuasi wa rais huyo walibubujikwa na mchazo baada ya uamuzi huo. |
Mahakama iliamuru kwamba alitoa nakala nyingi za siri ikiwa ni ukiukaji wa kiapo alichokula cha kulinda siri za serikali mbali na kukiuka sheria kwa kumruhusu bi Choi kuingilia maswala ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Mahakama ya juu nchini Korea kusini yamwondoa madarakani Rais Park Geun-hye
Reviewed by Zero Degree
on
3/10/2017 11:56:00 AM
Rating: