Loading...

Forbes: Orodha ya Matajari 10 wa Dunia, ..Bill Gates bado Kinara

Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kwa mara nyingine anaongoza orodha ya jarida la Forbes ya watu tajiri zaidi duniani mwaka huu.

Idadi ya mabilionea (wa dola) duniani imeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia 
2,043.

Kwa mujibu wa jarida hilo, mali ya Bw Gates imeongezeka hadi $86bn, kutoka $75bn.

Anafuatwa na Warren Buffett, aliyeongeza utajiri wake kwa $14.8bn hadi $75.6bn.

Rais wa Marekani Donald Trump, hata hivyoa meshuka nafasi 220 hadi 544 kwenye orodha hiyo ya matajiri na sasa ana mali ya $3.5bn pekee.

Forbes wamesema kushuka kwa utajiri wa Bw Trump kwa $1bn kulitokana na kuupungua kwa kasi ya sekta ya biashara ya ardhi na makao Marekani.

Katika orodha hiyo ya Forbes, mabilionea 183 walijipatia utajiri wao kupitia teknolojia, utajiri wao ukiwa jumla ya dola trilioni moja za Marekani.

Orodha hiyo imetawaliwa na mabilionea kutoka Marekani.

Wengine walio kwenye 10 matajiri zaidi ni mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye amepanda hadi nambari tatu utajiri wake ukiongezeka kwa kiwango cha juu zaidi kuliko wa mtu mwingine yeyote duniani.

Utajiri wake uliongezeka kwa $27.6bn hadi $72.8bn.

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg yupo nafasi ya tano na mwanzilishi mwenza wa Oracle Larry Ellison alikuwa nambari saba.

Idadi ya mabilionea duniani ambao sasa wanafikia 2,043, ilipata ongezeko kubwa zaidi kwa mwaka mmoja katika kipindi cha miaka 31 tangu orodha hiyo ianze kuandaliwa.

Mabilionea kutoka Marekani walikuwa 565, jambo ambalo Forbes wanasema huenda lilitokana na kuimarika kwa soko la hisa pakubwa tangu Trump aliposhinda uchaguzi Novemba 2016.

China ilikuwa ya pili kwa mabilionea ikiwa na mabilionea 319 nayo Ujerumani ya tatu na mabilionea 114.

Watu 10 matajiri zaidi:

  1. Bill Gates (mwanzilishi mwenza wa Microsoft): $86bn
  2. Warren Buffett (mwekezaji Mmarekani): $75.6bn
  3. Jeff Bezos (mwanzilishi wa Amazon): $72.8bn
  4. Amancio Ortega (mwanzilishi wa Inditex): $71.3bn
  5. Mark Zuckerberg (mwanzilishi wa Facebook): $56bn
  6. Carlos Slim (mfanyabiashara kutoka Mexico): $54.5bn
  7. Larry Ellison (mwanilishi mwenza wa Oracle): $52.2bn
  8. Charles Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
  9. David Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
  10. Michael Bloomberg (mwanzilishi wa Bloomberg): $47.5bn
Wanawake katika orodha hiyo waliongezeka hadi 227 kutoka 202, na wanamiliki jumla ya $852.8bn.

Kwa mwaka wa pili, Mfaransa Liliane Bettencourt, wa maduka ya bidhaa za urembo L'Oreal, alikuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na mali ya $39.5bn. Alirithi biashara hiyo.
Forbes: Orodha ya Matajari 10 wa Dunia, ..Bill Gates bado Kinara Forbes: Orodha ya Matajari 10 wa Dunia, ..Bill Gates bado Kinara Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 04:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.