Loading...

Ujenzi wa Reli ya kisasa kutoa ajira zaidi ya 6,000

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa inayotarajiwa kuanza kujengwa nchini, inatarajia kutengeneza zaidi ya ajira 6,000.

Kadogosa aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam na kufafanua kuwa kampuni hiyo itatoa ajira za moja kwa moja 200 kutoka kwa vijana wa vyuo vikuu nchini.

Alisema watu hao 200 miongoni mwao watakuwepo wahandisi, mafundi, makenika na wataalamu wengine wanaohusiana na masuala hayo ya rasilimali za reli.

Alisema wataalamu watakaotoka vyuo vikuu watakuwa wa kwanza kupata mafunzo kabla ya kujiunga na Rahco. Pia alisema mbali na kutengeneza ajira nchini ujenzi huo utatoa nafasi ya biashara kwa Watanzania.

“Hatua hii ya ujenzi wa reli itatengeneza ajira katika vituo vya biashara ambayo itatoa nafasi kwa Watanzania hususan vijana kutengeneza ajira mbalimbali,” alisema.

Katika hatua nyingine, Rahco imesisitiza kuwa waliovamia eneo la wazi la reli hiyo ni lazima waondoke haraka.

Akizungumzia malalamiko yaliyotolewa dhidi yao, alisema hatua ya kuwaondoa wavamizi hao waliojenga pembezoni mwa reli hiyo ilifuata sheria na miongozo.

“Waathirika wote walipewa notisi mwaka mmoja uliopita, na walikuwa wakikumbushwa kubomoa nyumba zao,” alisema na kusisitiza kuwa wote waliobomolewa ndani ya eneo hilo hawatapata fidia yoyote.

Alisema jumla ya nyumba 485 kutoa Dar es Salaam mpaka Pugu zilijengwa kimakosa katika eneo hilo la hifadhi ya reli.
Ujenzi wa Reli ya kisasa kutoa ajira zaidi ya 6,000 Ujenzi wa Reli ya kisasa kutoa ajira zaidi ya 6,000 Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 04:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.