Loading...

Simba yanasa kiungo matata Jijini Arusha

SIMBA si watu wa mchezomchezo, kwani baada ya kuona uwezo mkubwa wa kiungo wa Madini FC ya jijini Arusha, Awesu Awesu, haraka sana wakatafuta mawasiliano naye, lengo likiwa kumalizana naye kabla wapinzani wao hawajawazunguka mlango wa nyuma.

Hatua hiyo ya Simba kumdaka kiungo huyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri na kuwafanya viungo wa wekundu hao wa Msimbazi, Said Ndemla na Jonas Mkude, kutofanya vizuri kwa kiungo huyo.

Awesu alifanya kazi kubwa katika safu ya kiungo katika kikosi chake, hali iliyopelekea Simba kushindwa kufanya mashambulizi kutokana na umahiri wa kiungo huyo wa Madini.

Kuwapo kwa mchezaji huyo kuliifanya Simba kushindwa kuonyesha kiwango kizuri kutokana na umahiri mkubwa na kuwafanya viungo wa Simba kutopata nafasi ya kufanya mashambulizi.

Baada ya kuondolewa kwa mchezaji huyo, kuliwapa mwanya wachezaji wa Simba kupeleka mashambulizi na hatimaye kupata nafasi ya kufunga bao la ushindi lililofungwa na Laudity Mavugo.

Kitendo cha kufanya vizuri kwa kiungo huyo kimemshawishi Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, kumfuata na kuhitaji mawasiliano (namba ya simu) kwa ajili ya kuwa karibu.

DIMBA lilimtafuta mchezaji huyo, aliyesema ni kweli baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Hanspope alimfuata kutaka namba, huku akimhakikishia kumfuatilia kwa kila hatua.

“Ni kweli nilizungumza na huyo bosi, aliniambia nimpatie namba yangu ya simu kwa ajili ya kuwa karibu yangu, suala la kujiunga na Simba hajaniambia,” alisema.

Awesu alisema amehitaji ukaribu wake na kuhakikisha wanamfuatilia kwa kila hatua, kama Simba watahitaji huduma yake yupo tayari, akiamini kwamba anakwenda kucheza timu anayoishabikia.
Simba yanasa kiungo matata Jijini Arusha Simba yanasa kiungo matata Jijini Arusha Reviewed by Zero Degree on 3/21/2017 04:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.