Loading...

Hii hapa droo ya nusu fainali ya Kombe la FA, ..Chelsea yapangwa na Tottenham

Mahasimu wa jiji la London Chelsea na Tottenham wamepangwa kukutana katika nusu fainali Kombe la FA nchini Uingereza, Arsenal nao wakapangwa kukutana na Manchester City.

Arsenal watakuwa wanacheza nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29

Nusu fainali zote mbili zitachezewa Wembley wikendi ya 22 na 23.

Chelsea walifuzu kwa kuwafunga Manchester United 1-0 Jumatatu.

Spurs walifika nusu fainali kwa kulaza Millwall 6-0 Jumapili.

Arsenal, ambao walishinda kombe hilo 2014 na 2015 waliwalemea Lincoln City 5-0 Jumamosi.

Manchester City ambao wanacheza nusu fainali kwa mara ya kwanza katika misimu minne, walifuzu kwa kulaza Middlesbrough 2-0 ugenini.

Droo ya nusu fainali:

Chelsea vs Tottenham Hotspur

Arsenal vs Manchester City
Matokeo ya mechi kati ya Chelsea vs Tottenham na Arsenal vs Manchester City zilipokutana nusu fainali:
Chelsea v Tottenham
1 Machi, 2015:Chelsea 2-0 TottenhamKombe la Ligi
29 Nov, 2015:Tottenham 0-0 ChelseaLigi ya Premia
2 Mei, 2016:Chelsea 2-2 TottenhamLigi ya Premia
26 Nov, 2016:Chelsea 2-1 TottenhamLigi ya Premia
4 Jan, 2017:Tottenham 2-0 ChelseaLigi ya Premia
Arsenal v Manchester City
13 Sep, 2014Arsenal 2-2 Manchester CityLigi ya Premia
18 Jan, 2015:Manchester City 0-2 ArsenalLigi ya Premia
21 Des, 2015:Arsenal 2-1 Manchester CityLigi ya Premia
8 Mei, 2016:Manchester City 2-2 ArsenalLigi ya Premia
18 Des, 2016:Manchester City 2-1 ArsenalLigi ya Premia
Hii hapa droo ya nusu fainali ya Kombe la FA, ..Chelsea yapangwa na Tottenham Hii hapa droo ya nusu fainali ya Kombe la FA, ..Chelsea yapangwa na Tottenham Reviewed by Zero Degree on 3/14/2017 01:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.