Loading...

Matumaini ya kumalizika kwa mgomo wa madaktari nchini Kenya yaanza kuonekana.

Serikali ya Kenya imeridhia kusaini mkataba wenye mapendekezi mapya yaliyokuwa yakipiganiwa na madaktari wa Hospitali za Umma nchini humo na kuibua mgomo uliodumu kwa siku 100.

Pande za upatanishi zinazohusiska ni Wizara ya afya, viongozi wa kidini, Chama cha wanasheria, madaktari na Ofisi ya Mwanasheria mkuu ambapo wote kwa pamoja wamekubali kusaini stakabadhi husika kabla ya leo saa nane na nusu mchana ili kumaliza mgomo huo.

Viongozi wa Chama cha Madaktari KMPDU wanasema watatangaza rasmi wakati wowote usitishwaji wa mgomo punde tu sitakabadhi hizo za mkataba wa kurudi kazi zitakapo wasilishwa mahakamani kuidhinishwa na kuhalalishwa.

Baadhi ya mambo yanayoangaziwa kwenye mkataba huo ni madaktari kulipwa mishahara yao ya miezi mitatu waliokuwa kwenye mgomo,kutodhulumiwa wala kuchukuliwa hatua za kisheria kwa madaktari walioshiriki mgomo,kulewa asilimia hamsini ya nyongeza ya mishahara,kusajiliwa kwa mkataba wa CBA kwa kipindi cha siku kumi na nne na kuajiriwa kwa madaktari 1200 kila mwaka.
Matumaini ya kumalizika kwa mgomo wa madaktari nchini Kenya yaanza kuonekana. Matumaini ya kumalizika kwa mgomo wa madaktari nchini Kenya yaanza kuonekana. Reviewed by Zero Degree on 3/14/2017 01:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.