Loading...

Kauli ya Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi juu ya kadi nyekubdu ya Chirwa

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema hakuona tatizo lolote kuhusu goli la Chirwa ambalo lilikataliwa na mwamuzi Ahmed Simba aliyechezesha mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga.

“Referee ni binadamu, anaweza akafanya kakosa kama binadamu wengine lakini mimi sikuona haja ya kadi ya njano ya kwanza. Ile ya kudunda mpira sina matatizo nayo, kwa sababu mchezaji anatakaiwa aheshimu maamuzi ya referee lakini mchezaji kudunda mpira wakati mwamuzi ameshapiga filimbi ni kosa,” – Juma Mwambusi.

“Goli alilofunga Chirwa halafu likakataliwa lilikuwa ni clear goli lakini mwamuzi kwa mtazamo wake akaona si goli kwa sababu limefungwa kwa mkono lakini hata ukiangalia marudio kwenye TV inaonesha mchezaji kafunga lakini hakutumia mkono.”

“Kwa hiyo viongozi watakaa na kujadili jinsi ya kufanya ili kuona ni namna gani tunaepukana na hiyo ghasia iliyotupata.”

Chirwa alifunga goli akiunganisha kwa kichwa krosi ya Simon Msuva lakini mwamuzi alilikataa goli hilo kwa madai Chirwa alitumia mkono kufunga goli hilo, mwamuzi akamuonya Chirwa kwa kadi ya njano.

Muda mfupi baadae, mwamuzi alipuliza filimbi kwenye tukio ambalo lilimuhusisha Chirwa kumchezea rafu mchezaji wa Ruvu Shooting, Chirwa akaudundisha mpira kuashiria kutoridhishwa na maamuzi ya referee, mwamuzi akamuonesha kadi ya njano ya pili na kumsindikiza na kadi nyekundu.
Kauli ya Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi juu ya kadi nyekubdu ya Chirwa Kauli ya Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi juu ya kadi nyekubdu ya Chirwa Reviewed by Zero Degree on 3/02/2017 03:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.