Loading...

Kauli ya Zito baada ya Rais Magufuli kumtaka Makonda aendelee na kazi yake bila kujali ya mitandaoni

KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameonyesha kutofurahishwa na kauli ya Rais Magufuli kwa RC Makonda aliyoitoa leo wakati wa uzinduzi wa barabara za juu 'FlyOver' Ubungo Jijini Dar Es Salaam.

Rais Magufuli aliyasema:

“Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga.

Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Baada ya hayo zito Kabwe kwa kutumia ukurasa wake wa Facebook akaandika haya yafuatayo:

Mkuu wa Mkoa anavamia chumba cha habari binafsi Kwa mitutu ya Bunduki na Askari wa Umma. Wananchi wanalalamika kuhusu uvamizi huu ikiwemo Waziri, Wabunge, Wamiliki Wa vyombo vya habari na waandishi wenyewe.

Rais bila kumung'unya maneno anatamka hadharani kuwa Mkuu wa Mkoa aendelee na kazi zake. Hii maana yake ni kwamba Rais amemtuma Mkuu wa Mkoa kuvamia Chombo cha habari. 

Nawashauri wana habari wote kukutana kupitia MOAT, Jukwaa la Wahariri na Press Clubs na kuamua Kwa pamoja kususia kuandika habari zote za Serikali mpaka hapo Serikali
  1. Itakapolaani tukio hili na kuahidi kuwa halitotokea tena 
  2. Itakapochukua hatua kali dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.
Nakumbuka Sana Jukwaa la Wahariri chini ya Sakina Dewji-Datoo

Hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook:

Kauli ya Zito baada ya Rais Magufuli kumtaka Makonda aendelee na kazi yake bila kujali ya mitandaoni Kauli ya Zito baada ya Rais Magufuli kumtaka Makonda aendelee na kazi yake bila kujali ya mitandaoni Reviewed by Zero Degree on 3/20/2017 04:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.