Loading...

Mambo 5 ya kufahamu kuhusu waarabu wa Algeria watakaocheza na Yanga kwenye Kombe la Shikisho Afrika [Caf]

Mchana wa March 21 2017 shirikisho la soka barani Afrika CAF lilipanga ratiba ya timu 32 zitakazocheza mchezo wa mwisho wa mtoano kabla ya kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho Afrika, Yanga ilipanga kuanza kucheza nyumbani dhidi ya MC Alger ya Algeria.


KAMA NDIO UNAISIKIA MC ALGER YA ALGERIA KWA MARA YA KWANZA


1- MC Alger
kirefu chake ni Mouloudia Club d’Alger ambapo ilianzishwa mwaka 1921 nchini Algeria ni moja kati ya Club zenye historia kubwa Algeria ila kuanzia 1977 hadi 1986 ilikuwa ikijulikana kama Mouloudia Pétroliers d’Alger.

2- MC Alger sio timu ya kubeza hata kidogo sio kwa sababu viwango vya soka la Afrika Kaskazini vipo juu au Algeria ipo juu katika viwango vya FIFA lakini ndio Club ya kwanza ya Algeria kuwahi kushinda CAF Champions League mwaka 1976.

3- Ni moja kati ya vilabu vyenye mafanikio Algeria wamewahi kushinda Ligi Kuu ya Algeria mara 7 na mwaka 1976 ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kufuzu kucheza Club Bingwa Afrika baada ya kushinda Ligi Kuu Algeria na ilifanikiwa kufika hadi fainali ya michuano hiyo na kuifunga Hafia Conakry ya Guinea.
4- MC Alger ni Club inayotumia uwanja wa Stade Omar Hamadi uliyopo katika mji mkuu wa Algeria (Algers) timu hiyo hutumia jezi zenye rangi nyekundu na kijani.

5- Kwa sasa MC Alger ipo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Algeria unaoshirikisha timu 16, MC Alger iliyo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi imecheza mechi 20 imeshinda mechi 10, kufungwa mechi 5 na kutoka sare mechi 5.
Mambo 5 ya kufahamu kuhusu waarabu wa Algeria watakaocheza na Yanga kwenye Kombe la Shikisho Afrika [Caf] Mambo 5 ya kufahamu kuhusu waarabu wa Algeria watakaocheza na Yanga kwenye Kombe la Shikisho Afrika [Caf] Reviewed by Zero Degree on 3/22/2017 01:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.