Loading...

Marcel Desailly: Asilimia 71% ya dunia imejazwa na maji, asilimia 29% iliyobaki inajazwa na Ng'olo Kante

N'golo Kante adai kujisikia faraja na kufurahishwa na watu wanaozidi kumsifia msimu huu.

Kutokana kiwango cha hali ya juu alichoonyesha katika nafasi kiungo Chelsea, mashabiki na baadha ya wachezaji wa soka wa zamanu wameibuka kumsifia, na kuanzisha maada inayohusu 'Ukweli Kuhusu Kante'.

Marcel Desailly
 
Miongoni mwao alikuwa ni nyota wa zamani wa 'The Blues' kiungo Marcel Desailly ambaye ambaye alimtania Kante kwa kusema kuwa yeye (Kante) anachukua 29% ya dunia.



Ingawa Kante alifafanua kwamba si kweli, ni utani.

'Kiukweli nina furaha sana na kiwango changu msimu huu,' Kante alisema hayo kuelekea mechi ya kufuzu kombe la dunia ya Ufaransa dhidi ya Luxemburg na mechi ya kirafiki dhidi Hispania.

'Ni kweli nakupokea mengi ya kusifiwa na kwamba ni kitu kinachonishangaza na kunifanya nijisikie vizuri. Lakini si suala la kunichululia muda sana na kuathiri uwezo wangu. Jambo la muhimu ni kumaliza msimu huu vizuri.

'Wachezaji wenzangu wa Chelsea walinieleza juu ya hili linloitwa 'Ukweli kusu Kante'. Ni suala la kufurahisha. Ni wazi kwamba siwezi kujaza asilimia 30 ya uso wa dunia.

'Nilifanya uamuzi sahihi kuja Chelsea. Tuko katika nafasi nzuri na tunajitahidi kucheza mpira mzuri. '
Marcel Desailly: Asilimia 71% ya dunia imejazwa na maji, asilimia 29% iliyobaki inajazwa na Ng'olo Kante Marcel Desailly: Asilimia 71% ya dunia imejazwa na maji, asilimia 29% iliyobaki inajazwa na Ng'olo Kante Reviewed by Zero Degree on 3/22/2017 05:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.