Loading...

Mgao wa milioni 50 kwa kila kijiji kuanza mwezi April

Katibu Mtendaji wa Baraza na Uwezeshaji Wananchi (NEEC), Beng’i Issa [kushoto]
AHADI ya Rais John Magufuli ya kutoa fedha Sh milioni 50 kwa kila kijiji inatarajiwa kufika katika baadhi ya vijiji nchini kuanzia mwezi ujao na tayari Sh bilioni 59 zimekwishatengwa.

Utolewaji wa fedha hizo kwa kila kijiji ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015/2020 ambayo aliitoa mwaka juzi wakati akiwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza kupitia kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya TBC, Katibu Mtendaji wa Baraza na Uwezeshaji Wananchi (NEEC), Beng’i Issa alisema baraza limefikia hatua ya mwisho kabisa ya uratibu wa fedha hizo na kinachosubiriwa ni kibali kutoka serikalini kuhusu fedha hizo.

“Sisi kama baraza tumemaliza kutengeneza na kuratibu na kilichobakia ni hatua za mwisho kwa serikali kutoa kibali cha fedha hizo, zilizotengwa zitakwenda katika baadhi ya vijiji kupitia halmashauri, lakini vikundi vitakapopata ni vile vitakavyofikia vigezo,” alisema Issa na kuongeza kuwa vikundi hivyo viwe na uzoefu wa kuweka akiba na kukopeshana kwa ndani ya mwaka mmoja na kuendelea.

Kuhusu vigezo vya vikundi vitakavyopata fedha hizo ni vile ambavyo vinatoka katika kijiji husika, lakini pia halmashauri zitahusika kwa kuunda kamati na pia kuwepo kwa mratibu katika halmashauri husika atakayesimamia utekelezaji wa fedha hizo pamoja na kutoa elimu.
Mgao wa milioni 50 kwa kila kijiji kuanza mwezi April Mgao wa milioni 50 kwa kila kijiji kuanza mwezi April Reviewed by Zero Degree on 3/15/2017 12:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.