Loading...

Ndege yenye mwendo kasi zaidi duniani kutengenezwa

KUNDI la wataalamu wa usafiri wa anga wameweka wazi mpango wao wa kutengeneza ndege yenye mwendo kasi zaidi duniani itakayitwa Boom. Ndege hiyo itachukua nafasi ya ndege aina ya Concorde ambayo ilikuwa ndiyo yenye mwendo kasi zaidi.

Ndege hiyo aina ya Boom, itasafiri kwa kasi mara mbili na nusu zaidi ya ndege za kawaida kufikia mwendo wa mile 1,451 sawa na kilomita 2,335 kwa saa. Concorde ilikuwa ikisafiri kwa speed ya mile 1,350 sawa kilomita 2,170 na kwa saa.

Kwa mujibu wa wanasayansi hao, ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 40 kwenye mistari miwili na itawawezesha abiria wanaosafiri kutoka London kwenda New York Marekani kufika chini ya muda wa saa tatu na nusu. Ticket moja itagharimu Dola za Kimarekani 5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 11,158.

“Tunazungumzia ndege ya kwanza yenye mwendo kasi zaidi duniani ambayo watu wanaweza kumudu gharama zake,” mgunduzi wa ndege hiyo na Ofisa Mtendaji Mkuu Blake Scholl aliliambia gazeti la Guardin la Uingereza.

Anasema huu si muujiza wa sayansi, wanafanya kwa vitendo. Utaweza kusafiri kutoka London kwenda New York kwa saa tatu na nusu kwa gharama ya Dola za Marekani 5,000 tu ambayo ni karibu sawa na gharama za daraja la kibishara (Business class) kwenye ndege za kawaida.

Japokuwa Scholl alikubali kuwa wazo lake ni gumu kuaminika, aliwahakikishia watu wanaompinga kuwa wazo hili litatekelezwa kwa kutumia teknalojia zilizopo.

Kwa mujibu wa tovuti ya kampuni yake, itatumia malighafi zisizo na uzito mkubwa ambazo zinaiwezesha ndege hiyo kuwa na mwendo kasi kuliko ndege zote duniani.

“Tutatumia teknalojia zilizopo, tutakachofanya ni kuziweka katika namna ya tofauti kidogo ili kupata matokeo tofauti,” anasema.
Ndege hiyo bado ipo kwenye hatua za awali za matengenezo lakini lengo la kampuni ya Scholl ni kujaribu ndege ya kwanza mwishoni mwa mwaka huu katika mji wa Colarado.

Timu ya marubani, wahandisi wa ndege pamoja na wajenzi wanaohusika na ugunduzi wa ndege hiyo ya abiria, wameunda kampuni sita na watashiriki katika utengenezaji wa ndege 30.

Kampuni hiyo ilipata kuungwa mkono na kampuni ya Richard Branson's Virgin Group, ambayo ipo kwenye mchakato wa kutengeneza ndege ya abiria itakuyoruka anga za mbali. Kampuni hiyo pia imesaini mkataba wa kununua ndege 10 kwa matarajio ya kuanzisha safari ya muda mfupi kati ya London na New York baada ya safari za Concorde kusitishwa.

Scholl anasema ndege hiyo itaweza kuziba nafasi ya Concorde ambayo ilishindwa kujiendesha kutokana na gharama za nauli kuwa kubwa.

“Ni vigumu kuweza kupata abiria wa kutosha kwa gharama ya Dola za Marekani 20,000 kwa abiria mmoja, hii ndiyo sababu iliyowafanya Concorde kushindwa kuendelea kuwapo,” anasema Scholl.

Anaongeza: “Tutakachofanya ni kupunguza bei ya tiketi na kufanya ndege kuwa na saizi ya kawaida ili kutuwezesha kuruka kwa mwendo kasi zaidi.”

Gazeti la The Guardian la Uingereza pia liliripoti kwamba Scholl amesaini makubaliano na kampuni za ndege za Jiji la London ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kununua ndege hiyo itakayogharimu Dola za Marekani bilioni mbili.

Ndege yenye mwendo kasi zaidi duniani kutengenezwa Ndege yenye mwendo kasi zaidi duniani kutengenezwa Reviewed by Zero Degree on 3/24/2017 06:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.