Loading...

Ndugu wa familia moja waliokutwa na hatia ya ujangili wamehukumiwa kwenda jela miaka 12

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka 12 jela, kaka wawili wa familia moja waliopatikana na hatia ya ujangili wa meno ya ndovu.

Aidha, pamoja na kutupwa gerezani magari yao matatu yametaifishwa kwa kosa la kutumika kufanikisha ujangili.

Waliohukumiwa kifungo hicho ni Boniface Malyango maarufu kama ‘shetani hana huruma’ na Lucas Malyango maarufu kama ‘rukas mponze’ ambao ni miongoni mwa majangili waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na majangili, mahakama iliambiwa.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joseph Fovo, na kusisitiza kuwa wafungwa hao walitengeneza genge la uhalifu wa makosa ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na ujangili.

Alisema washtakiwa hao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kwanza na miaka miwili kwa mashitaka ya pili.

Awali akiwasomea mashitaka, wakili wa serikali Salimu Msemo, alisema walifanya kosa hilo kati ya Januari 2009 na Oktoba 23, 2015 walipotengeneza genge hilo la uhalifu.

Alisema kesi hiyo ilikuwa mashahidi 11 pamoja na vielelezo 15 yakiwamo magari matatu yaliyokuwa yakihusika katika uhalifu huo.

Aliyataja magari hayo kuwa ni pamoja na gari namba Mitsubishi Canter, Honda CRV na RAV 4 na kuitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa majangili wengine.

Aliiomba kutaifisha magari hayo chini ya kifungu cha 111(1)(d)(e) cha sheria ya uhifadhi wa wanyama pori ya mwaka 2009 kwa kuwa yalitumika kubebea meno na moja kati yao kufanikisha ujangili. Hakimu Fovo alikubali ombi la kutaifishwa kwa magari hayo ambayo ni mali ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Boniface.
Ndugu wa familia moja waliokutwa na hatia ya ujangili wamehukumiwa kwenda jela miaka 12 Ndugu wa familia moja waliokutwa na hatia ya ujangili wamehukumiwa kwenda jela miaka 12 Reviewed by Zero Degree on 3/04/2017 12:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.