Loading...

Orodha ya wanawake 20 matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2017 [Forbes]

Liliane Bettencourt ndiye mwanamke tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa Forbes
Katika orodha ya watu matajiri zaidi duniani ambayo imetolewa na jarida la Forbes, wanawake si wengi lakini idadi yao inaendelea kuongezeka.

Katika orodha ya mabilionea (wa dola za Marekani) ambayo ilitolewa Jumatatu, wanawake mabilionea duniani waliongezeka hadi 227 kutoka 202 mwaka uliotanguliwa.

Wanamiliki mali ya jumla ya $852.8bn. Isabel dos Santos kutoka Angola bado ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika, na utajiri wake unakadiriwa kuwa $3.1 bilioni.

Kwa mwaka wa pili, Mfaransa Liliane Bettencourt, 94, wa maduka ya bidhaa za urembo L'Oreal, ndiye mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na mali ya $39.5bn. Alirithi biashara hiyo.

Utajiri wake umeongezeka kwa $3.4bn kutoka mwaka jana. Katika orodha ya jumla ya mabilionea duniani, kwa sasa anashikilia nambari 14, ambapo ameshuka kutoka nambari 11 mwaka jana.

Bettencourt anamiliki theluthi moja ya hisa za L'Oreal pamoja na watoto wake.

Babake Eugene Schueller alianzisha kampuni hiyo mwaka 1907 na alifariki dunia 1957.

Mwanamke wa pili kwa utajiri duniani ni Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya $33.8bn, $1.5bn juu ya mwaka jana. Kwa jumla, anashikilia nambari 17.

Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani.

Utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.

Yeye ni miongoni mwa wanawake wanne wa familia ya Walton ambao wamo kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani, kwa pamoja utajiri wao ukiwa jumla ya $49.5 bilioni. Wanne hao ni Christy Walton, mjane wa kakake John, na binamu zake Anne Walter Kroenke na Nancy Walton Laurie.

Isabel dos Santos kutoka Angola ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika
Wanaokamilisha orodha ya wanawake 10 matajiri zaidi duniani ni wanawake wengine waliorithi utajiri wao ingawa huenda wasiwe wanafahamika sana duniani.

Ni pamoja na Jacqueline Mars, mwenye mali ya $27 bilioni na ambaye babu yake Frank Mars alianzisha kampuni ya pipi ya Mars Inc.

Mwingine ni Maria Franca Fissolo mwenye mali ya $25.2 bilioni ambaye baba mke wake alianzisha kampuni ya Nutella na mumewe marehemu Michele Ferrero alianzisha kampuni ya Ferrero Group. Kampuni ya Ferrero hutengeneza Ferrero Rocher, Kinder Chocolate na Tic Tacs.
Mjane wa Steve Jobs

Kadhalika, kuna mjane wa Steve Jobs, Laurene Powell Jobs, ambaye ana utajiri wa $20 bilioni kutokana na hisa zake katika kampuni za Apple na Disney.

Wengi wa wanawake matajiri duniani walirithi utajiri wao, Forbes wanasema.

Lakini pia wapo wafanyabiashara 15 wa kike ambao hawakurithi mali, sana kutoka Asia.

Mmoja ni Nguyen Thi Phuong Thao kutoka Vietnam anayemiliki kampuni ya safari za ndege ya VietJet.

Marekani, ambayo ina mabilionea wengi wanawake duniani, ina wanawake 74 mabilionea.

Ujerumani na Uchina zinafuata zikiwa na mabilionea 28 na 23 mtawalia.

Wanawake 20 matajiri zaidi duniani 2017

1. Liliane Bettencourt - $39.5bn

Chanzo cha Utajiri: L'Oreal

2. Alice Walton - $33.8bn

Utajiri: Wal-Mart

3. Jacqueline Mars - $27bn

Chanzo cha Utajiri: Pipi

4. Maria Franca Fissolo - $25.2bn

Chanzo cha Utajiri: Nutella, chokoleti

5. Susanne Klatten - $20.4bn

Chanzo cha Utajiri: BMW, dawa

6. Laurene Powell Jobs - $20bn

Chanzo cha Utajiri: Apple, Disney

6. Gina Ronehart - $15bn

Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini

8. Abigail Johnson - $14.4bn

Chanzo cha Utajiri: Usimamizi wa fedha

9. Iris Fontbona - $13.7bn

Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini

10. Beate Hesiter - $13.6bn

Chanzo cha Utajiri: Maduka ya jumla

11. Charlene de Carvalho-Heineken - $12.6bn

Chanzo cha Utajiri: Heineken

12. Blair Parry-Okeden - $12.2bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

13. Massimiliana Landini Aleotti - $9.5bn

Chanzo cha Utajiri: Dawa

14. Yang Huiyan - $9bn

Chanzo cha Utajiri: Biashara ya nyumba na ardhi

15. Katharine Rayner - $8.1bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

16. Margaretta Taylor- $8.1bn

Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari

17. Zhou Qunfei: - $7.4bn

Chanzo cha Utajiri: Skrini za simu za kisasa

18. Pauline MacmMillan Keinath - $6.8bn

Chanzo cha Utajiri: Cargill

19. Sandra Ortega Mera - $6.7bn

Chanzo cha Utajiri: Zara

20. Carrie Perrodo - $6.3bn

Chanzo cha Utajiri: Mafuta
Orodha ya wanawake 20 matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2017 [Forbes] Orodha ya wanawake 20 matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2017 [Forbes] Reviewed by Zero Degree on 3/22/2017 11:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.