Polisi waanza kumsaka aliyemtolea bastola Nape Nnauye
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso |
- Agizo la Waziri Mwigulu Nchemba kwa aliyemtishia Bastola Nape Nnauye
- Mkutano wa Nape wazuiwa Protea, ...azungumza na wanahabari chini ya ulinzi wa polisi
- Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ....Nape 'Out', Mwakiembe kujaza nafasi yake
- Nape alivyojitabiria kuvuliwa uwaziri wa habari
Hayo yalisemwa jana na Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso. Awali, Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu alitafutwa, lakini simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyemtaka mwandishi amtafute Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ili atoe ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa agizo la Waziri Nchemba.
Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba.
Alipopigiwa simu, Senso alijibu kwa ufupi kuwa wameanza kufanyia kazi agizo la Waziri Nchemba.
- Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa athibitisha Rais kumteua Dk. Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye
- Mimi ndio chanzo kikubwa cha Nape kuvuliwa uwaziri, Gwajima
Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya polisi aliyevalia kiraia kumtishia bastola, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM).
Waziri Nchemba alilaani kitendo hicho na kumuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kuchukua hatua “Mheshimiwa Nape sio jambazi, hana rekodi za uhalifu. Kitendo cha kutolewa bastola si cha Kitanzania na si cha kiaskari na sio cha Kimungu,” ameandika Mwigulu katika ukurasa wake wa facebook.
“Kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera, nawaza mbali, ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini. Nimemuagiza IGP achukue hatua.
“Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania. Nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari, basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”
Source: Mwananchi
Polisi waanza kumsaka aliyemtolea bastola Nape Nnauye
Reviewed by Zero Degree
on
3/25/2017 10:38:00 AM
Rating: