Zaidi ya n'gombe 100 wamekufa mkoani Pwani ikisadikika kuwa wamekunywa maji yenye sumu.
Zaidi ya n'gombe 100 wamekufa baada ya kunywa maji yanayosadikika kuwa na sumu katika mgodi wa Ashiraf unaochimba na kusaga kokoto katika kijiji cha Pongwe Msungura kata ya Msata halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani.
Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wafugaji wamesema tukio hilo ni mara ya pili kutokea ambapo mara ya kwanza mbuzi zaidi ya 70 walikufa huku wakiomba serikali kutowapa vibali wawekezaji wa kupasua mawe na kusaga kokoto katika maeneo yaliyotengwa kwa ajiri ya malisho ya mifugo huku wakisema wakati wa upasuaji wengine upata majeraha kutokana na mawe kuruka katika maeneo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mh. Alhaji Majidi Mwanga ambaye amefika katika eneo hilo na kutoa maagizo kwa wafugaji kuwa na uvumilivu wakati vyombo vya usalama vikifanya uchunguzi wa kuchukuwa sampo na kupeleka kwa mkemia mkuu wa serikali huku akiagiza jeshi la polisi kumsaka na kumkamata mmiliki wa mgodi huo ambaye akuwepo katika maeneo hayo hili kutoa ushilikiano wa tukio hilo.

Source: ITV
Zaidi ya n'gombe 100 wamekufa mkoani Pwani ikisadikika kuwa wamekunywa maji yenye sumu.
Reviewed by Zero Degree
on
3/22/2017 11:24:00 PM
Rating: