Zanako FC yailazimisha Klabu ya Yanga sare ya 1-1 Taifa
Zanako FC wameilazimisha Yanga sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa taifa katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.
Yanga bado haijautumia vizuri uwanja wa taifa kwa sababu katika mechi mbili za klabu bingwa msimu huu ambazo wamecheza kwenye uwanja wa taifa, mechi zote wametoka sare ya kufungana 1-1 (Yanga 1-1 N’gaya Club na Yanga 1-1 Zanaco).
Yanga watasafiri kwenda Zambia kucheza mechi ya marudiano inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi ijayo huku Zanaco wakiwa ni wenyeji wa mchezo huo.
Yanga wakiwa kwenye uwanja wa taifa wamelazimishwa sare ya pili kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na N’gaya Club ya Comoro.
Simon Msuva alianza kuifungia Yanga goli la kuongoza dakika 39 kipindi cha kwanza baada ya Ngoma kumpasia Justine Zulu ambaye aliuweka mpira kwenye njia Msuva akaukuta na kuunganisha kwa mguu wake wa kushoto kuiandika Yanga bao.
Kipindi cha pili Zanaco walibadilika na kuanza kufanya mashambulizi mengi golini kwa Yanga wakitumia upande wa kulia wa mabingwa hao watetezi wa VPL upande ambako alikuwa akicheza Hassan Ramadhani ‘Kessy’.
Dakika ya 77 Zanaco walipata bao la kusawazisha lililofungwa na Attram Kwame akiwa pekeake kwenye nje kidogo ya sita baada ya kupigwa mipira miwili mirefu ambayo mabeki wa Yanga walishindwa kuidhibiti.
Matokeo hayo sio mazuri kwa upande wa Yanga kwa sababu watalazimika kupata ushindi wa magoli yoyote au sare ya kuanzia magoli mawili na kuendelea ili kufuzu hatua inayofata.
Matokeo hayo sio mazuri kwa upande wa Yanga kwa sababu watalazimika kupata ushindi wa magoli yoyote au sare ya kuanzia magoli mawili na kuendelea ili kufuzu hatua inayofata.
Yanga bado haijautumia vizuri uwanja wa taifa kwa sababu katika mechi mbili za klabu bingwa msimu huu ambazo wamecheza kwenye uwanja wa taifa, mechi zote wametoka sare ya kufungana 1-1 (Yanga 1-1 N’gaya Club na Yanga 1-1 Zanaco).
Yanga watasafiri kwenda Zambia kucheza mechi ya marudiano inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi ijayo huku Zanaco wakiwa ni wenyeji wa mchezo huo.
Zanako FC yailazimisha Klabu ya Yanga sare ya 1-1 Taifa
Reviewed by Zero Degree
on
3/11/2017 11:55:00 PM
Rating: