Loading...

AJALI: Daladala yagonga Treni na kusabisha kifo cha mtu mmoja jijini Dar

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya basi la abiria almaarufu daladala, lenye namba za usajili T435 DGG linalofanya safari zake kutoka Gongo la Mboto kwenda Mnazi Mmoja jijini hapa kuigonga Treni ya Pugu, Saa 11 alfajiri ya jana, Aprili 19, 2017 katika makutano ya reli na Barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 10:50 alfajiri kwenye makutano ya reli na Barabara ya Nkrumah jijini hapa. Baadhi ya abiria waliokuwamo kwenye daladala hiyo, walisema kabla ya ajali kutokea, walipiga yowe kumtaka dereva asivuke reli hadi treni ipite, lakini alikaidi.

Majeruhi ambaye amelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi), Emmanuel Ngowi (25), mkazi wa Ukonga Mizizini aliyevunjika mguu wa kulia, alisema dereva wa daladala alipuuza na kuamua kuvuka.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli, Simon Chilery alimtaja abiria aliyefariki dunia kuwa ni mwanamume na kwamba, majeruhi wanane walipelekwa Hospitali ya Amana na wengine 15 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).


Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa dereva ambaye alipofika relini, licha ya kuoneshwa ishara ya kusimama kupisha treni hiyo, alishindwa kulimudu gari na kusababisha aligonge treni hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, kati ya majeruhi 23 wa ajali hiyo, wanane wapo Hospitali ya Amana na wengine 15 wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), huku watatu kati yao wakiwa na hali mbaya.
AJALI: Daladala yagonga Treni na kusabisha kifo cha mtu mmoja jijini Dar AJALI: Daladala yagonga Treni na kusabisha kifo cha mtu mmoja jijini Dar Reviewed by Zero Degree on 4/20/2017 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.