Loading...

Uhamiaji yatoa siku 90 kwa raia wa kigeni nchini

Anna Makakala, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imetoa siku 90 kwa wageni kufanya uhakiki wa vibali vya ukaazi ili kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi nchini pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala baada ya uzinduzi wa mfumo wa uhakiki kwa kutumia njia ya kielekroniki amesema mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa waajiri na wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na mamlaka husika.

Dkt. Makakala amezitaka taasisi na mashirika binafsi baada ya kuhakiki vibali vya wageni wao watatakiwa kuwasilisha taarifa za vibali hivyo katika ofisi za Idara ya Uhamiaji za mikoa zilizopo karibu na ofisi zao.



Uhamiaji yatoa siku 90 kwa raia wa kigeni nchini Uhamiaji yatoa siku 90 kwa raia wa kigeni nchini Reviewed by Zero Degree on 4/20/2017 10:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.