Loading...

Huu ndio ujumbe wa Frank Lampard kwa John Terry

Baada ya John Terry kutangaza kuachana na Chelsea mwisho wa msimu huu, watu wengi wameguswa na jambo hilo lakini mmoja kati ya maswahiba wa karibu sana wa Terry ambae ni Frank Lampard naye limemgusa.

Wakati Lampard anatangaza kustaafu soka, John Terry aliandika sana kuhusu historia yake na Lampard na jinsi atakavyomkumbuka katika maisha yake kama mchezaji lakini pia kama rafiki yake wa karibuu.

Sasa Lampard nae ameandika “Mchezaji mkongwe kuwahi kuwa na mafanikio makubwa ndani ya Chelsea, nina faraja sana kuwahi kucheza na beki bora kama wewe katika premier league”

“Nadhani wewe ni beki bora kuliko yeyote niliyewahi kumuona, uliiongoza klabu ndani na nje ya uwanja na ukaifanya timu iwe bora huku ukipambana katika masuala ya ushindi na kuiletea heshima Chelsea”

“Wewe ni bora sana, sio kwa sababu ya kipaji chako tu bali pia kwa sababu unavyopenda mafanikio ndani na nje ya uwanja, hakika unapaswa kuheshimiwa”

“Hakika wewe ni captain mwenye mafanikio zaidi katika historia ya timu huku nje ya uwanja ukiwa rafiki mwema kabisa sio tu kwangu ila kwa kila mtu hata walioko nje ya Chelsea’

“Msaada wako kwa watu wengi hauhesabiki, umefanya vitu vingi sana ambavyo kila mtu hawezi kuviona na nakutakia mafanikio mema ila naamink siku zote utaipenda Chelsea na itakuheshimu” alimalizia Lampard.
Huu ndio ujumbe wa Frank Lampard kwa John Terry Huu ndio ujumbe wa Frank Lampard kwa John Terry Reviewed by Zero Degree on 4/19/2017 12:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.