Loading...

Mbwa alivyookoa maisha ya watu wengi kwa kumzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga nchini Nigeria

Mbwa mmoja aliokoa maisha ya watu wengi wakati ya sherehe ya harusi mjini Maiduguri nchini Nigeria, kwa kushambulia mwanamke moja mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Inaarifiwa kuwa mwanamke huyo alijaribu kuingia katika sherehe hiyo ya harusi, kwa mujibu wa kituo cha redio cha jeshi.

Mbwa huyo pamoja na mshambuliaji wa kujitoa mhanga wote walikufa wakati msichana huyo alilipua bomu alipokuwa akimkimbia mbwa huyo.


Polisi wanasema kuwa mbwa huyo alimilikiwa na mwenyeji wa eneo ambapo sherehe hiyo ya harusi ilikuwa ikifanyika.
Mbwa alivyookoa maisha ya watu wengi kwa kumzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga nchini Nigeria Mbwa alivyookoa maisha ya watu wengi kwa kumzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga nchini Nigeria Reviewed by Zero Degree on 4/05/2017 02:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.