Loading...

Rais amewaapisha Makatibu Wakuu wapya, Mabalozi na Kamishna wa TRA

Rais John Magufuli amewaapisha viongozi aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali akiwamo Profesa Kitila Mkumbo, aliyeteuliwa jana kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Wengine walioapishwa na Rais leo ni Dk Leonard Douglas Akwilapo (Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia)

Wengine ni Dk Ave Maria Semakafu (Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia) na Baraka Haran Luvanda ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Kwa upande wake, Sylvester Ambokile ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Charles Edward Kichere ameapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia viongozi hao wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha.




Rais amewaapisha Makatibu Wakuu wapya, Mabalozi na Kamishna wa TRA Rais amewaapisha Makatibu Wakuu wapya, Mabalozi na Kamishna wa TRA Reviewed by Zero Degree on 4/05/2017 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.