Loading...

Aubameyang alivyoleta balaa Dortmund

BILA shaka umeshazoea kumwona Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia mabao yake huku akiwa amevalia ‘mask’ usoni.

Lakini kwa hali ilivyo sasa, unaweza usimuone tena Mgabon huyo akifanya hivyo mpaka atakapoondoka Dortmund. Unajua kwanini?


Klabu ya Borrusia Dortmund imetangaza kumpiga Aubameyang faini ya pauni 43,000 kwa kosa la kusherehekea bao akiwa amevalia ‘mask’ kwenye mchezo dhidi ya Schalke.

Hatua hii inakuja baada ya kampuni ya Puma inayodhamini klabu hiyo kuchukizwa na kitendo cha Aubameyang kuvalia mask yenye nembo ya washindani wao, kampuni ya Nike.

Taarifa ya Puma ilisema: “Tunashangaa sana namna wapinzani wetu wanavyoweza kufanya kitendo hiki kwa mchezaji.”

Aubameyang (27), amekuwa na kawaida ya kushangilia mabao yake kwa staili ya kuvalia ‘mask ya Spiderman au Batman’ lakini safari hii amejikanyaga baada ya kuchanganya bidhaa hizo mbili za kampuni moja wakati akishangilia.

Kwenye mchezo dhidi ya Shalke alikofunga bao lake la 24 msimu huu, Mgabon huyo alionyeshwa kadi ya njano kwa kitendo hicho.

Baada ya taarifa hii, Aubameyang aliposti kwenye mtandao wake wa Instagram: “Mimi ni mjinga? Acheni utani, hivi ndivyo nilivyozoea kuishi, haya ni maisha yangu!

“Hii ni dunia yangu na napenda watoto wapende kutazama mchezo wa soka.

Lakini kocha wa Dortmund, Thomas Tuchel, yeye aliamua kukaa upande wa straika wake na kumtetea kwa kitendo hicho.

“Tunachanganywa sana na hili suala la ushangiliaji wake wa kuvaa mask ya Batman au Spiderman, lakini kwa upande wangu nafikiri hili ni jambo linalomfanya ajitume zaidi uwanjani.

“Uongozi unaweza kuchukua maamuzi yake ya kiutawala lakini kama benchi la ufundi tuko pamoja naye na tunaendelea kumsapoti kwa kila hali.

“Aubameyang amejitangaza muda mrefu katika hili na litakuwa jambo la ajabu kama tukiweka ngumu kuzikatisha juhudi zake.”

Tuchel amemshauri Aubameyang kukubali adhabu hiyo na kuendelea kujituma kwa ajili ya mashabiki wake wa Dortmund.

“Mnaweza kusema maneno mengi mabaya kwa kitendo chake, lakini nina amini yeye ni mchezaji mkubwa anayejitambua. Nitazungumza naye na tunategemea ataendelea na kasi yake ya upachikaji mabao.

“Namjua vyema, hili ni jambo dogo sana kwake na ninaamini atalimaliza kwa njia nzuri na kulinda sifa yake ya mchezaji wa kulipwa.”
Aubameyang alivyoleta balaa Dortmund Aubameyang alivyoleta balaa Dortmund Reviewed by Zero Degree on 4/05/2017 01:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.