Namna agizo la Kikwete lilivyoondoka na mabilioni ya fedha
Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete. |
Aidha, agizo hilo limebainika kukamilisha miradi mingi ya maendeleo iliyokuwa imepangwa kutekelezwa katika bajeti kwa miaka ya fedha 2013/14 na 2014/15.
Novemba 4, 2012, Kikwete, maarufu JK, aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini, kujenga maabara kwa kila shule ya sekondari katika kipindi cha miaka miwili kuanzia siku hiyo.
JK alitoa agizo hilo alipohutubia wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi mkoani Singida, waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Itigi.
Alisema maabara za sayansi ni muhimu katika maendeleo ya wanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo. JK alisema kutokana na umuhimu huo, kulikuwa kunahitajika ushirikiano kama ule ulioonyeshwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari za kata ulioanza mwaka 2006.
Hata hivyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imekosoa utaratibu huo na kufichua ufujaji wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na watendaji wa halmashauri na kukwamisha utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo, wakidai pesa zimeelelekezwa kwenye ujenzi wa maabara.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vedasto Ngombale, ndiye aliyefichua kadhia hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini hapa.
Alisema kuwa kutokana na tamko hilo la JK, watendaji wa halmashauri walilazimika kuelekeza kwenye ujenzi wa maabara fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi mingine ya maendeleo, huku baadhi yao wakipata mwanya wa kufuja fedha za umma kwa kisingizio kwamba wamezielekeza kwenye utekelezaji wa agizo la Rais.
"Kilichotokea lile lilikuwa tamko, lakini katika maeneo mengi hapakuwa na bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo," Ngombale alisema.
"Kama unavyofahamu, ili kutekeleza mradi wowote katika serikali, sharti kwamba mradi huo utajwe kwenye bajeti, lakini Mheshimiwa Kikwete, kwa mamlaka aliyokuwa nayo, akatoa tamko la utekelezaji wa jambo hilo.
"Sasa kilichotokea ni kwamba baada ya tamko lile, watendaji wa halmashauri kwa maana ya wakurugenzi watendaji, walichokifanya ni kuchukua pesa kutoka katika kasma mbalimbali kuhakikisha kwamba wanatengeneza maabara.
"Na matokeo yake, tulipokuja kupitia yale mahesabu baada ya utekelezaji, kukawa kumebainika kuna ufujaji mkubwa wa pesa katika halmashauri nyingi."
Ngombale ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema licha ya tamko hilo kusababisha kutumika kwa mabilioni ya shilingi yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwamo ya maji, mpaka sasa bado kuna halmashauri nyingi hazijakamilisha ujenzi wa maabara, akiitolea mfano halmashauri ya Kilwa anayotoka.
Zipo halmashauri nyingi ambazo bado hazijakamilisha ujenzi wa maabara hali ya kwamba tamko hilo lilitolewa na utekelezaji ulifanyika kwa kuchukua pesa kutoka katika mafungu tofauti tofauti," alisema Ngombale.
Mtoto huyo wa kaka mdogo wa mwanasiasa mkongwe, Kigunge Ngombale Mwiru, alisema agizo hilo la JK lilitolewa bila kuwa na bajeti, hivyo fedha za miradi mingine zilikuwa zinachukuliwa na kuingizwa kwenye ujenzi wa maabara, kinyume cha sheria ya bajeti ya mwaka husika.
"Lakini, katika utekelezaji huo, ndiyo mwanya wa matumizi mabaya ya pesa ulipatikana na sisi tulivyokagua, tumeona ni kiasi gani. Kuna ufisadi mkubwa," alisema.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Gazeti la Nipashe na Mwenyekiti wa LAAC Ngombale yaliyofanyika kwenye jengo la Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bunge. Endelea...
Swali: Je, kuna uwezekano wa wahusika wa ufujaji huo kuchukuliwa hatua za kisheria kupitia Takukuru na pengine kutakiwa kurejesha fedha?
Ngombale: Uwezekano huo upo. Kamati yangu imeshatoa maagizo ilipopitia baadhi ya halmashauri.
Uzoefu ni ule ule, unapotoa tamko kwamba kitu fulani kifanyike bila ya kuwa na bajeti, unawalazimisha watendaji wa halmashauri wafanye hivyo. Wao wanapata wapi hizo pesa? Kinachotokea ni kuchukua pesa kutoka katika kasma mbalimbali kutekeleza lile lililoagizwa.
Na kama unavyofahamu, tamko linaendana na muda na tamko hili lilitolewa na kiongozi wa juu kabisa wa serikali.
Kila mtu atahangaika kwa kila namna ili ahakikishe kwamba lile tamko linatekelezwa kwa muda. Katija kufanya hivyo, matokeo yake ni ufujaji mkubwa wa pesa za umma maana wengine wanatumia mwanya huo kujipatia fedha wakiwa tayari wameshapata sababu za kuziambia mamlaka za ukaguzi zinapohoji matumizi ya fungu husika.
Swali: Ni halmashauri zipi ambazo ziliongoza kwa kadhia hiyo katika ukaguzi uliofanywa na LAAC?
Ngombale: Kwa ujumla, tatizo hilo lipo katika halmashauri zote nchini na taarifa yetu inaeleza. Mfano, katika ujenzi huo wa maabara Halmshauri ya Kinondoni ilitumia Sh. bilioni 2.281, Urambo Sh. milioni 786.632, Mlele Sh. milioni 725.916, Ngara Sh. milioni 267.143, Rorya Sh. milioni 206.875 na Hai Sh. milioni 200.
Kumbuka hapakuwa na bajeti ya ujenzi wa maabara na fedha hizo zilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo lakini zikabadilishwa matumizi kinyume cha sheria na watu wakapata mwanya wa kuzipiga.
Swali: Je, kiasi hicho cha fedha kingetumika kufanyia nini?
Ngombale: Hizi ni zile pesa ambazo zinatolewa kwa halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ya maji na barabara. Zilitumika vibaya sana. Katika kila halmashauri tuliyopitia, tuligundua kuwa zile pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zilichukuliwa na kuelekezwa kwenye maabara. Pesa hizi ni za mwaka 2013/14 na 2014/15.
Swali: Azma ya kila shule kuwa na maabara inawezekana au ndiyo inabaki kuwa alama ya ufisadi wa fedha za umma kwa kuwa gharama za jengo ni ndogo kuliko za vifaa ili kuwa maabara halisi?
Ngombale: Azma hii kama ingekuwa na mpango mkakati, inawezekana. Mafanikio ya suala lolote ni mipango ya maana na si mipango ya zimamoto kama hii tunayoiona katika haya maagizo. Katika baadhi ya shule, agizo hili limetekelezwa.
Tumefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika baadhi ya halmashauri ikiwamo Manispaa ya Lindi Mjini wiki mbili zilizopita. Lindi Mjini ni miongoni mwa halmashauri ambazo utekelezaji wa ujenzi wa maabara umefanyika vizuri. Karibu shule zote zina maabara na tulitembelea shule moja, siikumbuki kwa jina, kwa kweli maabara zile zimejengwa vizuri.
Shida kubwa kwa halmashuri nyingi ni kwamba majengo yenyewe hayajakamilika, 'installation' (usimikaji) ya vifaa ni hatua ya mwisho. Majengo hayajakamilika, shule nyingi za kata bado hazina maabara. Naona kama nguvu ya lile tamko imekwisha. Sasa hivi kuna programu nyingine tu zinaendelea.
Msisitizo tena wa maabara ni kama haupo. Tamko lilitolewa, waliotekeleza, wametekeleza lakini walio wengi bado hawajatekeleza na pesa nyingi za serikali zimepotea.
Swali: Katika uongozi wako LAAC, changamoto zipi hasa zinakukumba ukizingatia ni mara yako ya kwanza kuongoza kamati hii nyeti?
Ngonbale: Changamoto kubwa ni mawanda ya utendaji wetu wa kazi. Kama unavyofahamu, katika bajeti ya mwaka huu, Mfuko wa Bunge uliminywa, kwa hiyo utendaji wetu wa kasi pia ulibanwa.
Tunafanya kazi kwa namna tatu; kwanza tunawaita watendaji wa serikali za mitaa na mahesabu yao, tunakuja kuwakagua mezani. Namna ya pili ni sisi kwenda kukagua miradi ya maendeleo na namna ya tatu tunapitia tu ile taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) na sisi tukawa 'tume-comment' (tumetoa maoni yetu).
Sasa 'this time' (safari hii) tumekwenda kukagua miradi ya maendeleo ili kuangalia thamani ya matumizi ya fedha. Tulichogundua miradi mingi ya maendeleo utekelezaji wake uko chini.
'Interest' yetu hasa mwaka huu ilikuwa kwenye miradi ya maji. Karibu asilimia 90 ya miradi ya maji tuliyoenda kuikagua tumegundua ilikuwa na dosari. Mradi unaweza ukawa umekamilika lakini hautumiki, tumebaini hili kwa miradi mingi.
Pia tumebaini mradi umepewa pesa nyingi lakini utekelezaji wake ni kama haupo. Jingine ni kwamba ushirikishwaji wa jamii katika miradi hiyo ya maji haupo.
Unakuta jamii ya watumiaji wa mradi husika hawajui chochote kuhussu mradi wenyewe. Kwa kifupi, kuna changamoto kubwa kwenye miradi ya maendeleo na hasa miradi ya maji.
Swali: Kutokana na ukata unaolikabili Bunge, kamati yako imepata semina yoyote ya mafunzo katika mwaka huu wa fedha?
Ngombale: Ni ukweli kwamba hali ya Bunge kifedha si nzuri. Tulipata semina moja tu, ilifanyika mwaka jana. Kwa ujumla, bado kamati haijajengewa uwezo wa kufanya kazi. Bado tunahitaji tupate semina nyingi zaidi.
Tulikuwa tunatarajia tupate semina kutoka kwa wenzetu wa CAG, lakini kama unavyofahamu, CAG naye ana matatizo ya kifedha. Bajeti yake ya mwaka huu wa fedha imetekelezwa kwa kusuasua, hapakuwa na 'flow' (mtiririko) nzuri ya fedha.
Tuna tatizo kubwa la kupata semina za kuwawezesha wajumbe wa kamati kuwa na uwezo mkubwa wa kuhoji matumizi ya fedha za serikali.
Swali: Unawezaje kujigawa kutekeza majukumu ya kamati hii nyeti na ya ubunge?
Ngombale: Hilo linawezekana kwa sababu tunafanya vikao vya kamati nje ya ratiba za vikao vya Bunge. Lakini pia tunapokuwa kwenye kamati, tunafanya shughuli zetu kwa muda fulani, muda mwingine unabaki kwenda kufanya shughuli zingine za kibunge ingawa nayo ni ngumu kidogo.
Inahitaji kujitoa kwa sababu kama kamati ingekuwa inafanya kazi kama inavyotakiwa, maana yake ingekuwa inatumia muda mwingi kukagua miradi ya maendeleo karibu nchi nzima. Lakini kutokana na hali hii sasa, tumekosa fursa ya kukagua miradi mingi zaidi ya maendeleo.
Ukweli ni kwamba ili tuweze kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, kamati inatakiwa ikakague miradi 'physically' (kutembelea eneo husika).
Hii ya kuletewa mezani, mara nyingi unaweza kujikuta tunapingwa changa la macho kwa kuwa zile ni namba tu. Lakini unapokwenda 'physically', unaona pesa zilizotolewa na utekelezaji wenyewe uliofanyika. Kwa ujumla, tunajitahidi kwa kadri tunavyoweza kufanya hizo kazi.

Source: Nipashe
Namna agizo la Kikwete lilivyoondoka na mabilioni ya fedha
Reviewed by Zero Degree
on
4/24/2017 11:21:00 AM
Rating: