Loading...

Rais mpya wa Caf atunukiwa tuzo ya heshima

SERIKALI ya Madagascar imempa tuzo ya heshima ya kitaifa, Rais wa Shirikisho la Afrika (Caf), Ahmad Ahmad, kama heshima baada ya kutwaa nafasi hiyo kubwa kwenye uongozi wa soka la Afrika.

Rais wa Madagascar, Hery Rajaonarimampianina, katika taarifa yake rasmi ya kiserikali alisema kwamba ushindi wa Ahmed ni wa taifa zima hivyo tuzo aliyompa ni chachu kwa yeye kufanya vizuri kwenye uongozi wa soka la Afrika.

“Hii ni heshima kubwa kwa nchi, tumeweza kushinda kama taifa na wala si jambo la mtu mmoja. Tuna imani kwamba tutafanikiwa pamoja kama nchi na si Ahmed peke yake,” alisema Rais Hery.

Ahmed (57), alimshinda mtangulizi wake, Issa Hayatou kwa kura 34 dhidi ya 20 alizopata mpinzani wake kwenye nafasi hiyo ya uongozi wa Caf.
Rais mpya wa Caf atunukiwa tuzo ya heshima Rais mpya wa Caf atunukiwa tuzo ya heshima Reviewed by Zero Degree on 4/09/2017 06:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.