Loading...

Serikali yataifisha Kiwanda cha nyama mkoani Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack
Serikali ya mkoa wa Shinyanga imelazimika kukifunga kiwanda cha nyama cha Shinyanga na kukirudisha serikalini rasmi baada mmiliki anayetambulika kwa jina la 'TRIPLE S' kushindwa kukiendesha na kukiuza kinyemela kwa kampuni ya Agro Ranch ya Kagera hali ambayo imesababisha uchakavu wa majengo na mashine baada ya kutokutumika kwa zaidi ya miaka 40.


Maamuzi hayo yametolewa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi.Zainab Telack muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa na kamati ya ulinzi na usalama na kushuhudia uchakavu majengo huku baadhi ya mashine zilizokuwepo katika kiwanda hicho wakati akikabidhiwa mmiliki huyo miaka kumi iliyopita zikiwa hazijulikani zilipo huku zikidhaniwa zimeuzwa kinyemela.

Akizungumza kwa niaba ya Agro Ranch, Bw.Samweli Kombe amesema hajui chochote juu ya kuuzwa kwa mali za kiwanda na umiliki wa Agro Ranch kutoka 'TRIPLE S' huku baadhi ya nyaraka zikionyesha bado umiliki wa kiwanda ni wa mwekezaji anayeitwa 'Triple s'.

Katika hatua nyingine Bi.Zainab Telack amewataka wananchi waliolima katika maeneo ya kiwanda kuvuna mazao yao baada ya kukomaa na kuyaachia huku akimuagiza mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kata ya Old Shinyanga kuhakikisha baada ya mavuno hakuna mwananchi atakayeingia katika eneo la kiwanda.
Serikali yataifisha Kiwanda cha nyama mkoani Shinyanga Serikali yataifisha Kiwanda cha nyama mkoani Shinyanga Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 04:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.