Loading...

Spika wa Bunge aagiza kukamatwa kwa Freeman Mbowe na Halima mdee.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ameagiza kukamatwa kwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe na mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ili wafikishwe kwenye kamati ya maadili kinga na madaraka ya Bunge kutokana na kudaiwa kutumia lugha za matusi wakati wa uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki.

Spika Ndugai amefikia hatua hiyo baada ya mbunge Kangi Lugola kuomba mwongozo kwa spika kuhusiana na madai ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge ambao walitoa lugha za matusi bungeni Mh.Spika ameagiza kwamba mh halima mdee akamatwe popote alipo na ikiwezekana apelekwe bungeni akiwa amefungwa pingu.

Source: ITV
Spika wa Bunge aagiza kukamatwa kwa Freeman Mbowe na Halima mdee. Spika wa Bunge aagiza kukamatwa kwa Freeman Mbowe na Halima mdee. Reviewed by Zero Degree on 4/06/2017 01:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.