Loading...

TCRA yazitoza faini kampuni za simu nchini kwa kutoa huduma mbovu

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imezitoza faini ya zaidi ya shilingi milioni mia sita kampuni zote za simu nchini kutokana na kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za mwaka 2011.

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, akizungumza jijini Dar es Salaam,ameyataja makampuni hayo kuwa ni kampuni ya Benson Informatics limited smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar telecom limited Zantel, Mic Tanzania limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania telecommunications company limited, TTCL huku akieleza kanuni zilizokiukwa.

Aidha Mhandisi Kilaba amesema fedha hizo wanatakiwa kuzilipa kabla ya mei 12 mwaka huu na kuziagiza kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma zinazokidhi ubora wa huduma za mawasiliano na kwamba wataendelea kuwachukulia hatua wale wanaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma.

Baadhi ya makampuni yaliyokumbwa na adhabu hiyo nao wamezungumzia namna walivyoipokea na kuelezea jitihada wanazofanya kuhakikisha wanafikia ubora unaotakiwa na zaidi.
TCRA yazitoza faini kampuni za simu nchini kwa kutoa huduma mbovu TCRA yazitoza faini kampuni za simu nchini kwa kutoa huduma mbovu Reviewed by Zero Degree on 4/13/2017 07:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.