Loading...

Ushauri wa Kaimu Jaji mkuu, Prof. Ibrahim Juma kwa Chama cha Mawakili Tanganyika [TLS]

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma (kushoto) akiwa na Rais John P. Magufuli
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameutaka uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania ili chama hicho kichangie katika utekelezaji wake.

Profesa Juma aliyasema hayo jana ofisini kwake ofisini kwake jijini Dar es Salaam alipotembelewa na uongozi wa TLS ukiongozwa na Rais wake, Tundu Lissu.

KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma
Alisema kuusoma na kuuelewa Mpango Mkakati huo, kutaifanya TLS kujua Mahakama inatoka na kuelekea wapi hususani katika maboresho ya utoaji haki nchini.

Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016- 2019/2010) umegawanyika katika nguzo kuu tatu ambazo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau.

Kwa upande wake, Lissu alisema lengo la kufika kwake ni kujitambulisha na pia kumpa pongezi kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Ushauri wa Kaimu Jaji mkuu, Prof. Ibrahim Juma kwa Chama cha Mawakili Tanganyika [TLS] Ushauri wa Kaimu Jaji mkuu, Prof. Ibrahim Juma kwa Chama cha Mawakili Tanganyika [TLS] Reviewed by Zero Degree on 4/01/2017 01:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.