Loading...

VIDEO: Manchester United ilivyonusurika kichapo Old Trafod

Ashley Williams akionyeshwa Kadi nyekundu katika mchezo huo, kadi iliyosababisha penati ilichezwa na Ibrahimovic
Mashetani wekundu wa Manchester wamendelea na mwendo wa kukuasua katika ligi kuu ya England baada ya kuambulia sare ya goli 1-1 na Everton katika dimba la Old Traford.

Beki wa Everton Phil Jagielka ndie aliyeanza kuzifumania nyavu za Man United katika dakika ya 22, ya mchezo kabla ya Zlatan ibrahimovic kusawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika za lala salama.

Leicester City wakicheza katika dimba lao la king power walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland kwa mabao ya Islam Slimani na Jamie Vardy.

Wanajeshi wa wa njano wa Watford wakaibuka na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi ya West Bromwich, mabao ya Watford yakifungwa na Troy Deeney na Mbaye Niang.

Nao Burnley wakataka nyumbani kwa ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya Stoke City.


VIDEO: Manchester United ilivyonusurika kichapo Old Trafod VIDEO: Manchester United ilivyonusurika kichapo Old Trafod Reviewed by Zero Degree on 4/05/2017 12:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.