Loading...

Zaidi ya kaya 3,000 ziko katika hatari ya kukumbwa na bomoabomoa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege Ilemela

Kaya zaidi ya 3,000 za mitaa minne ya kata ya Shibula wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, zilizojengwa ndani ya eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza,ziko hatarini kubomolewa ili kupisha mradi mkubwa wa upanuzi na ukarabati wa uwanja huo unaofanywa na mkandarasi kampuni ya Beijing Engineering Construction ya China kwa gharama ya shilingi bilioni 105.

Kaya hizo zipo katika mitaa ya Kihili,Nyamwilolelwa, Bulyanhulu na Shibula. Wananchi wa mitaa hiyo wamepinga kuondolewa bila kulipwa fidia.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Shibula Moshi Nzilwa amedai kuwa mpaka baina ya uwanja wa ndege wa Mwanza na eneo la Mlimani kwenye mtaa huo una walakini.

Oktoba 3 mwaka jana, Mkuu wa wilaya ya Ilemela ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Dk. Leonard Masale aliunda kikosi kazi cha wataalam wa kushughulikia migogoro ya mipaka ya ardhi baina ya taasisi za umma, maeneo ya jeshi na wananchi wa mitaa ya kata za Kahama, Kiseke, Shibula, Ilemela, Nyasaka,Shibula na Bugogwa.

Ripoti ya kikosi kazi hicho inayowahusisha wataalam wa ardhi kutoka Manispaa ya Ilemela, mamlaka ya uwanja wa ndege wa Mwanza na makao makuu ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) inatarajiwa kuwasilishwa kwa mkuu wa wilaya ya Ilemela.

Source: ITV
Zaidi ya kaya 3,000 ziko katika hatari ya kukumbwa na bomoabomoa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege Ilemela Zaidi ya kaya 3,000 ziko katika hatari ya kukumbwa na bomoabomoa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege Ilemela Reviewed by Zero Degree on 4/11/2017 07:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.