Loading...

Arsenal kumkosa Koscielny na Gabriel kwenye fainali ya FA dhidi ya Chelsea Jumamosi

Beki wa Arsenal Gabriel hatoshiriki katika fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya kupata jeraha litakalomweka nje kwa wiki nane.


Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyebebwa katika machela na kutolewa uwanjani katika mechi ya ushindi dhidi ya Everton, siku ya Jumapili anauguza jeraha la goti.
Laurent Kolscieny akipewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Everton baada ya kucheza kinyume na taratibu za uwanjani
Beki mwenza Laurent Koscielny pia naye hatoshiriki mechi hiyo ya fainali baada shirikisho la soka nchini Uingereza FA kukataa rufaa ya kadi nyekundi dhidi ya Everton.

Beki mwengine wa tatu wa Arsenal Shkodran Mustafi hajulikani iwapo atacheza.

Mustafi anaugua tatizo la mshtuko baada ya kupigwa kichwani wakati wa mechi dhidi ya Sunderland.


Katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano, Arsene Wenger alithibitisha kwamba Gabriel hatocheza hadi mwezi Agosti.

Aliongezea kuwa anasubiri maafisa wa matibabu kubaini hatma ya Mustafi iwapo anaweza kucheza.
Arsenal kumkosa Koscielny na Gabriel kwenye fainali ya FA dhidi ya Chelsea Jumamosi Arsenal kumkosa Koscielny na Gabriel kwenye fainali ya FA dhidi ya Chelsea Jumamosi Reviewed by Zero Degree on 5/24/2017 03:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.