Loading...

Azam FC wamethibitisha kuachana na John Bocco

Baada ya mitandao ya kijamii kuandika kuwa mshambuliaji wa Azam FC John Bocco amejiunga na Simba, taarifa ambazo bado hazina uhakika wowote, jana Mei 26 Azam FC wamethibitisha kuachana na John Bocco.

Azam FC kupitia kwa afisa habari wake Jafari Idd Maganga wameweka wazi kuwa John Raphael Bocco hatoendelea kuitumikia Azam FC kuanzia msimu ujao kutokana na mchezaji huyo kumaliza mkataba wake.

Jafari Idd kupitia SportExtra ya Clouds FM amethibitisha kuwa John Bocco sio mchezaji wao tena hivyo swali au ishu yoyote inayomuhusu John Bocco atafutwe mwenyewe.
Azam FC wamethibitisha kuachana na John Bocco Azam FC wamethibitisha kuachana na John Bocco Reviewed by Zero Degree on 5/27/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.