Loading...

Utabiri wa Michael Ballack wa Fainali ya Kombe la FA kati ya Arsenal na Chelsea

Kuelekea Fainali ya kombe la FA kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea, mmoja wa nyota wa zamani wa Chelsea ametoa utabiri wake.

Arsenal na Chelsea watapambana wikendi ya leo kwenye fainali ya FA na 'The Gunners' watakuwa na hamu ya kumaliza msimu walau kwa kubeba kikombe kimoja wakiwa na kocha wao Arsene Wenger wakati, Chelsea wakihitaji kubeba kikombe cha pili kwa msimu huu.

Utabiri wa Michael Ballack - Arsenal Vs Chelsea:

Ballack akiwa Chelsea
Akizungumza na kituo cha redio cha 'Newstalk' cha nchini Ireland kuhusiana na fainali hiyo ya FA, kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, Michael Ballack alisema:

“Chelsea kwa ufupi ndio chaguo langu lakini Arsenal nao wana ari nzuri na wamepata nguvu ya kucheza kwa umoja tena.

“Huu ni mchezo mmoja kwa wao kutafuta namna ya kumaliza msimu vizuri kwa kuwapa moyo mashabiki wa timu yao kufuatia kushindwa kuingia nne bora.”

Michael Ballack yeye, anatabiri hivi: Arsenal 0-1 Chelsea.
Utabiri wa Michael Ballack wa Fainali ya Kombe la FA kati ya Arsenal na Chelsea Utabiri wa Michael Ballack wa Fainali ya Kombe la FA kati ya Arsenal na Chelsea Reviewed by Zero Degree on 5/27/2017 12:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.