Loading...

BreakingNews: Kamati ya Maadili Bungeni imekubali kumsamehe Halima Mdee

Kamati ya Maadili ya haki na madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha taarifa za matukio mbalimbali ambazo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kuwaita wahusika kuwahoji kwa kukiuka kanuni za bunge.

Baadhi ya viongozi hao walitoa lugha chafu bungeni katika uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki lililofanyika Aprili 4 mwaka huu.

Sambamba na kosa la kutumia lugha hizo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, aliomba msamaha mbele ya Bunge kwa kumkosea Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai . Hatimae leo wabunge wamesamehewa na Bunge pamoja na kupewa onyo baada ya kukiri makosa yao.

Waliosamehewa na kamati hiyo ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge April 4, 2017. Mbunge mwingine ni Ester Bulaya ambaye amepewa karipio baada ya kukiri kosa lake. Wabunge hap walisimama bungeni na kuomba msamaha.

Kufuatia zoezi hilo la wabunge kumuombea radhi, Bunge liliazimia kuwa kiongozi huyo asamehewe na kupewa masharti kuwa endapo akifanya kosa lolote lingine bungeni atachukuliwa hatua na spika Ndugai. Bunge limeazimia mbunge huyo kuendelea na vikao vya bunge kama kawaida.
BreakingNews: Kamati ya Maadili Bungeni imekubali kumsamehe Halima Mdee BreakingNews: Kamati ya Maadili Bungeni imekubali kumsamehe Halima Mdee Reviewed by Zero Degree on 5/02/2017 02:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.