Loading...

Fainali ya Ligi ya EUROPA ni Manchester United na Ajax

United wamepata nafasi ya kutinga fainali kwa mara ya kwanza baada ya jana kutoka suluhu ya bao moja kwa moja dhidi ya Celta Vigo ya nchini Hispania.


Fainali hiyo itafanyika tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Friends Arena.

Katika mchezo huo timu zote zilimaliza pungufu uwanjani baada ya Eric Bailly kwa upande wa United na Rocanglia wa Celta Vigo kuoneshwa kadi nyekundu ikiwa imebaki dakika moja kwa mchezo kumalizika.

United walianza kupata bao dakika ya 17 baada ya Fellaini kuunganisha kwa kichwa mpira wa Marcus Rashford na bao hilo kuifanya United kwa mara ya kwanza kufunga mabao 100 katika msimu mmoja tangu mwaka 2012/2013.

Dakika zikiwa ximebaki 5 kufikia dakika ya 90 Celta Vigo walisawazisha bao hilo kupitia kwa Sebastian Rocanglia ambaye dakika 4 baadae alipewa kadi nyekundu.

Suluhu imewafanya United kifudhu kucheza fainali kwa jumla ya mabao 2 kwa 1 kutokana na ushindi wao wa kwanza walioupata ugenini wiki iliyopita.

Fainali hii ni ya 14 kwa kocha wa United Jose katika mashindano yote toka aanze ukocha lakini rekodi yake ikiwa nzuri kwani katika fainali 13 alizowahi kufika, ameshindwa fainali 2 tu kubeba ubingwa.
Fainali ya Ligi ya EUROPA ni Manchester United na Ajax Fainali ya Ligi ya EUROPA ni Manchester United na Ajax Reviewed by Zero Degree on 5/12/2017 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.