Loading...

Juventus yatinga fainali ya UEFA baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Monaco

Juventus imekua timu ya kwanza kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa ulaya (UEFA) baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa.

Magoli yote ya Juve yalifungwa kipindi cha kwanza, Mario Mandzukic aliifungia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 33 na jingine likiwa ni la Dani Alves katika dakika ya 44.

Mbappe ndiye aliyekuwa mfungaji wa goli la Monaco katika dakika ya 69 kwa usaidizi wa Moutinho.

Kwa matokeo hayo Juve imefanikiwa kutinga fainali ya UEFA kwa goli 4-1 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezewa Ufaransa.
Juventus yatinga fainali ya UEFA baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Monaco Juventus yatinga fainali ya UEFA baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Monaco Reviewed by Zero Degree on 5/10/2017 12:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.