Loading...

Chelsea walivyomaliza Ligi Kuu ya Uingereza kibabe

Chelsea wamevunja rekodi ya Ligu kuu ya Uingereza kwa ushindi katika msimu kwa kuifunga Sunderland goli 5-1 na kuweza kupata ushindi wa 30 kwa msimu huu.


Magoli kutoka kwa Willian, Eden Hazard, Pedro, Michy Batshuayi (2) yaliweza kuifanya Chelsea imalize msimu kwa kujibebea ubingwa kwa njia ya aina yake, na kutengeneza historia kwa Nahodha John Terry ambaye amefikisha mechi ya 717 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Kwa ushindi wa 30 wa msimu, Chelsea wamevunja rekodi iliyowekwa na Jose Mourinho alipoipa Chelsea Ubingwa katika misimu ya 2004/05 na 2005/06 ambapo katika misimu yote miwili Chelsea ilifanikiwa kumaliza kwa kushinda mechi 29 kati ya 38 za Ligi.

Ushindi huo unamaanisha kwamba Chelsea inamaliza Ligi Kuu ya Uingereza kama Bingwa na jumla ya pointi 93.


Chelsea walivyomaliza Ligi Kuu ya Uingereza kibabe Chelsea walivyomaliza Ligi Kuu ya Uingereza kibabe Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 11:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.