Wazee kutolipa kodi ya majengo
Picha ya Mtandaoni |
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuwaweka kando ulipaji wa kodi ya majengo wazee wa miaka 60 wenye nyumba moja na nyumba za ibada.
TRA imetoa muda siku 39 kuanzia juzi hadi Juni 30 mwaka huu kwa wadaiwa wa kodi ya majengo kulipa kabla operesheni ya kuwasaka kuanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza juzi, Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema watakaoshindwa kulipa hadi muda huo watatozwa faini isiyopungua Sh75,000 kulingana na thamani ya nyumba.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliyehudhuria mkutano huo aliwataka wakazi wa Mwanza kujenga utaratibu wa kulipa kodi kwa hiari.
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha aliishauri TRA kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

Reviewed by Zero Degree
on
5/24/2017 10:36:00 AM
Rating: