Loading...

Cristiano Ronaldo ameamua kuweka hadharani picha ya mapacha wake, itazame hapa!

Cristiano Ronaldo akiwa na mpenzi wake wa sasa Georgina Rodriguez
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ameamua kuwaweka wazi watoto wake mapacha ambao amewapata hivi karibuni.

Ronaldo ameamua kuwaweka wazi mapacha wake hao mitandaoni baada ya hapo jana kuthibitisha kupata watoto hao wakati timu yake ya taifa ya Ureno ilipotolewa kwenye michuano ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa.


“Ninafuraha sana kwa kuwabeba wapenzi wengine wawili wa maisha,” ameandika mchezaji huyo kwenye picha hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram.

Watoto hao wanaungana na kaka yao Cristiano Jr mwenye miaka saba. Wakati huo huo mpenzi wa Ronaldo, Georgina Rodriguez ambaye ni mwanamitindo anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitano.
Cristiano Ronaldo ameamua kuweka hadharani picha ya mapacha wake, itazame hapa! Cristiano Ronaldo ameamua kuweka hadharani picha ya mapacha wake, itazame hapa! Reviewed by Zero Degree on 6/30/2017 10:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.