Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 07



MTUNZI: MC Short Charles Gwimo

Ilipoishia..........Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwangu ingawa kwa upande mwingine ilikuwa ni ya maudhi hasa kwa kitendo cha kunyweshana mate eti ni denda. Furaha ilizidi kwa suala zima la ubadilishaji wa mlo kwa siku hiyo vinginevyo ningeungana na wenzangu kwenye kundi letu la wala ugali na maharage kavu kavu. Tulianua nguo zetu tukaagana na wapenzi wetu ingawa mimi sijatamkiwa au kutamka chochote kuhusiana na mapenzi zaidi ya kulishana denda. Ila ninafahamu kuwa matendo katika mapenzi yana nguvu zaidi kuliko maneno. Tuliagana kwa mabusu moto moto huku tukipeana miadi ya kukutana tena maeneo hayo hayo kwa kula bata na kujuana zaidi.


Endelea nayo: Viunga vyote vya shule vilitawaliwa na nyemi mithili ya mwanamke aliyevishwa pete ya uchumba kwa kushtukizwa. Vikundi mbalimbali vya sanaa za maonesho viliendelea kutumbuiza kwenye maeneo tofauti ya shule kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kutukaribisha vijana wa kidato cha kwanza. Nilijiunga na kikundi cha ngonjera kilichokuwa kikiongozwa na kijana wa ‘totozi’ yaani Mood. Kwa kuwa kikundi chetu hakikuwa na mwalimu wa kututungia, hapo ndipo nilipoamua kukionesha kipaji change cha utunzi wa mashairi na ngonjera. Tulijitokeza vijana kama watano ivi ambao tulihisi kuwa miongoni mwetu mmoja angeteuliwa ili aweze kulitungia eneo hilo. Tulipewa dakika nne nee kwa minajili ya kutoa wasifu wetu katika fani ya utungaji. Ilipofika zamu yangu sikupoteza muda hata chembe ya dakika zaidi ya kushuka beti kama kumi na tano zenye maswali na majibu mujarabu jambo ambalo liliwafanya walimu na wanafunzi wenzangu wanipe asilimia zote na Baraka za utungaji wa kipengele cha ngonjera. Baadhi ya vipande nilivyotiririka navyo ni kama:-

Kwa bibie kama mimi, Elimu ni kitu gani

Kwa asili ya umbo langui, Kazi nitaipata

Kwanza kuuza baa, Na pili huduma kwa gesti

Wenye pochi wataniandama, Kama malikia wa urembo

Uzuri ni tabibu, Kwa mabosi wa misongo

Yote uliyobaini, Yamepitwa na wakati

Umalaya siyo dili, Elimika mwanakwetu

Mwili msifanye soko, Daladala za ujiji

Magonjwa leo ni mengi, Ukibeep yanapiga

Majuto ni mjukuu, Ni kauli za wahenga.

*********

Nilitumia mtindo wa takhimisa katika kughani ngonjera zangu ili niwavunje wapinzani wangu ambao walilalia kughani kwenye mtindo wa tarbia, yaani ule wa mistari mine. Baada ya usaili huo kukamilika, nilianza kupokea marafiki wengi kwa lengo la kutaka kujenga urafiki na mimi na kutaka kupata anuani yangu na sahihi kwenye shajara zao. Vijana wenzangu walianza kunihusudu na kutaka tuanzishe kikundi cha maonesho shuleni kwetu. Kwa ujumla kina langu lilizagaa kona zote za Kigoma hasa katika sekondari nah ii ilianza kunipatia maraiki kwa kila shule. Maandalizi ya sherehe yaliendelea kwa ushindani mkubwa huku kikundi chetu cha ngonjera kikitia for a kwa kuwa na watazamji wengi kuliko vikundi vingine, jambo lililokolezwa na manjonjo yangu na kijana wa ‘totozi’ Mood.

*********

Jumamosi ya mwisho wa mwezi April iliwadia kama jua la Mashariki linavyochomoza. Muktadha wote wa shule ulitawaliwa na ugeni maridhawa. Wanafunzi takribani mia moja hamsini kutoka shule ya sekondari ya wasichana wakiongozwa na matroni wao nao walikuwa ni miongoni. Zilikuwa ni sura tofauti zenye kufanana kwa asilimia Fulani ingawa zilitofautiana kwa majina tu. Kama ni uchaguzi basi hao walichaguliwa kuiwakilisha vema shule yao. Kulikuwepo na wale wenye “English figure” na wale wenye maumbo ya kibantu yaliyosheheni miguu ya bia na makalio tepwe tepwe na yenye mvuto kwa baadhi ya wanaume wakware. Haya ni makalio ambayo watu wengi wameyapa maneno ya dhihaka kama vile “Hamsini hamsini, mia” au “Singida Dodoma, Singida Dodoma”.

*********

Sherehe zilianza rasmi mnamo saa nne asubuhi katika bwalo la chakula huku mgeni rasmi akiwa ni mzee wa fasihi na mkuu wa mkoa muheshimiwa Yusuf Migozi. Michezo mbalimbali ilichezwa mbele ya mgeni rasmi huku kila mwanamichezo akitamba na kughani kwa sifa ili ajiwekee rekodi ya kuokota dodo chini ya msufi kwa kuchaguliwa na mmoja kati ya vimwana walioalikwa. Kikundi chetu cha ngonjera ndicho kilichofungia dimba la michezo yote kabla ya kukaribishwa kwa mgeni rasmi ili atoe hotuba yake. Hakika kikundi chetu kilitunzwa zawadi mbalimbali kwa kila mtu kutunukiwa kilichomstahili. Miongoni mwa vitu tulivyotunukiwa ni pamoja na pesa, maua na vimemo. Tulipohitimisha kughani ngonjera, mgeni rasmi naye hakuzificha hisia zake kwa kutumwagia beti mbili za nguvu jambo ambalo liliufanya ukumbi mzima kulipuka kwa vigelegele. Vionjo vyake vilikuwa hivi:-


Mapenzi kizungumkuti, Hayaliwi kama biskuti

Yakipandiwa kwa kuti, Mwisho wake hatihati

Yakikosa mkakati, Huwa kama vichapati

Mapenzi kwa wanafunzi, Yawe mwiko abadani

Biashara Singarambe, Bungoma nchi jirani

Mwili msifanye soko, biashara Buguruni

Ni uvundo wa maisha, Pembe nne masikani

Ukitaka poteza dira, Chumvi tia kwenye chai.

*********

Mgeni rasmi alituasa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya, utoro wa darasani na tusiyavamia mapenzi katika umri mdogo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuyafumania mapenzi na kuwa FUMANIZI LA MAPENZI. Alihitimisha hotuba yake kwa kuwaonya vijana wenye mtindo wa kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwa kuwaambia athari zake ambazo ni kulegea kwa misuli ya mwaranda au kupata kansa ya mlango wa haja kubwa. Na hapa alikuwa anawazungumzia mabasha walioibuka shuleni kwetu ingawa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja.

====>>Itaendelea wiki ijayo...

Usiikose SEHEMU YA 08>>> ya Riwaya hii ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 07 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 07 Reviewed by Zero Degree on 6/23/2017 10:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.