Loading...

Ajali ya Lori imesababisha vifo vya watu zaidi ya 80 katika Jamhuri ya Afrika ya kati CAR

Picha ya Mtandao
Ajali ya lori moja la mizigo huko Jamhuri ya Afrika ya kati CAR imesababisha vifo vya zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa wakielekea sokoni mjini Bambari.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa limebeba watu wengi na kujazwa mizigo kupindukia huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi wakati lilipopenduka.

Maafisa wa trafiki wamelaumiwa kwa kutochukua hatua kuzuia ukiukwaji huo wa sheria za barabarani.
Ajali ya Lori imesababisha vifo vya watu zaidi ya 80 katika Jamhuri ya Afrika ya kati CAR Ajali ya Lori imesababisha vifo vya watu zaidi ya 80 katika Jamhuri ya Afrika ya kati CAR Reviewed by Zero Degree on 7/06/2017 10:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.